Tuesday, October 4, 2016

SBL KUWAPATIA MAJI BURE WAKAZI 65,000 WA TEMEKE, ARUSHA


Moja ya Mradi wa maji uliodhaminiwa na SBL Wilaya ya Hanang mkoani Manyara
 
Takribani wakazi 65,000 wa maeneo ya Temeke mkoani Dar es Salaam na Likamba mkoani Arusha hivi karibuni wataanza kufurahia upatikanaji wa maji safi na salama bure huduma ambayop itatolewa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo SBL imesema iko mbioni kujenga na kukabidhi miradi miwili ya maji katika maeneo ya Likamba na Temeke kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 170 ili kupunguza changamoto za uhaba wa maji unaowakabili wakazi wa maeneo hayo mawili.

Mkurugenzi wa Mahusioano SBL John Wanyancha amesema katika taaifa hiyo kuwa miradi hiyo miwili ya maji ni sehemu ya programu ya kampuni hiyo ya kusaidia jamii inayojulikana kama Maji kwa Uhai ambayo inalenga kuzipatia jamii nchini upatikanaji rahisi na wa uhakika wa maji safi na salama.

Kwa mujibu wa Wanyancha zaidi ya Watanzania milioni moja wameshanufaika na programu hiyo katika kipindi cha miaka minnne iliyopita kupitia miradi ya maji kama hiyo iliyotekelezwa katika mikoa ya Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma.

Mradi wa Maji kwa Uhai unajumuisha uchimbaji wa kisima pamoja na mfumo wake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua (sola) na tenki la maji ambapo kiasi cha lita 45,000 za maji huzalishwa kila baada ya saa sita.

“Kwa miaka kadhaa sasa tumeshuhudia maisha ya familia na kaya yakibadilika kijamii na kiuchumi kutokana na miradi hii ya maji hususani wasichana na wanawake ambao hawatumiii tena saa nyingi kutafuta maji safi. Badala yake muda huo hivi sasa wanautumia kuhudhuria shule pamoja na kufanya shughuli nyingine muhimu za uzalishaji,” alisema mkurugenzi huyo.

Mkakati wa kusaidia jamii wa SBL pia unalenga kutoa msaada kielemu kwa watoto wanaotoka katika familia maskini, uhifadhi wa mazingira, kuhamasisha unywaji wa pombe kistaarabu na kuwasaidia wakulima wa ndani kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha ambayo hadi sasa imewasaidia wakulima nchini kwa kuboresha maisha yao na maisha ya jamii.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu