Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Mwanza,  Ernest Makale, akitoa taarifa ya kukamatwa kwa mwanamke aitwaye Felister Mathias Mawe, kwa tuhuma za kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ  na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata  nafasi ya kujiunga na jeshi hilo kupitia maofisa anaofahamiana nao.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Mwanza,  Ernest Makale, akitoa taarifa ya kwa wanahabari kuhusu kukamatwa kwa  mwanamke aitwaye Felister Mathias Mawe, kwa tuhuma za kujifanya askari  wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini  Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ kupitia maofisa  anaofahamiana nao.
Mtuhumiwa Felister Mathias Mawe, anayetuhumiwa kujifanya askari wa Jeshi la  Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili  awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ.
Kushoto ni mtuhumiwa Felister Mathias Mawe, anayetuhumiwa kujifanya askari wa  Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini  Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ. Kulia ni Sophia Chacha ambaye ni mstaafu wa JWTZ anayetuhumiwa kumsaidia mtuhumiwa huyo kwa kumuunganisha na watu waliokuwa wakihitaji kujiunga na JWTZ.

Na BMG

Makale ameeleza kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kujipatia kiasi cha  shilingi 240,000 kati ya shilingi 500,000 alizokuwa ameomba kutoka kwa  mmoja wa walioomba kujiunga na JWTZ.

Amebainisha kwamba mtuhumiwa mmoja ambaye ni mstaafu wa JWTZ aitwaye Sophia Chacha  amekuwa akimsaidia mtuhumiwa huyo kwa kumuunganisha na watu waliokuwa  wakihitaji kujiunga na jeshi ambapo ili kupata nafasi hiyo mtuhumiwa  amekuwa akihitaji kiasi cha shilingi 500,000.

Mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 10 mwaka huu katika hoteli moja iliyopo Kirumba Jijini Mwanza kufuatia mtego wa maofisa wa TAKUKURU.

"Kitendo cha mtuhumiwa kujifanya afisa wa jeshi hakihusiani na makosa yaliyo  chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namaba 11/2007, hivyo  jalada lenye tuhuma hiyo namba PCCB/MZ/ENQ/40/2016 limehamishiwa kwa  wakili wa serikali mfawidhi ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani  kujibu tuhuma zinazomkabili". Alifafanua Makale.

Aidha Makale ameongeza kwamba TAKUKURU wilayani Misungwi imemfikisha  mahakamani Katibu wa Idara ya Utumishi wa Waalimu TSD wilayani humo kwa  kosa la tuhuma za kupokea rushwa shilingi 400,000 kutoka kwa Kitoki  Mgaya ili asimchukulie hatua za kinidhamu kazini.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: