Wednesday, October 12, 2016

WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI WATAKIWA KUWA MABALOZI WA ELIMU YA MPIGA KURA

Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Bi. Fausta Mahenge akitoa elimu ya mpiga kura kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria yanayosimamia chaguzi za Tanzania kwa wanafunzi 743 wa Shule ya Sekondari Kidinda wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Afisa Uchaguzi wa NEC Bw. Stephen Elisante akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kidinda wakati akitoa elimu ya Mpiga Kurra kwa wanafunzi wa shule hiyo, Bariadi mkoani Simiyu.

Na.Aron Msigwa – NEC, Bariadi-SIMIYU.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wanafunzi wa shule za Sekondari waliopatiwa elimu ya Mpiga Kura katika maeneo mbalimbali nchini kuwa mabalozi wazuri wa kuifikisha elimu waliyoipata kwa jamii inayowazunguka.

Wito huo umetolewa na Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bi. Fausta Mahenge wakati akitoa elimu ya mpiga Kura na kuhusu masuala ya kisheria na utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kidinda Bariadi mkoani Simiyu.

Amewaeleza wanafunzi hao kuwa NEC imezindua programu ya kuwafikia wanafunzi wa Shule za Sekondari na vyuo Vikuu ambayo haikuwepo hapo awali ili kuwafikia vijana wengi zaidi kwa kuzingatia nafasi ya vijana katika kufikisha elimu hiyo katika ngazi ya familia, mitaa na vijiji.

“Baada ya elimu hii nawaomba muwe mabalozi wa elimu ya mpiga kura katika maeneo yenu, ninajua ninyi mmetoka katika mitaa na vijiji mbalimbali, mkawe mabalozi wa kuelezea kazi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ngazi za familia zenu ili tusaidiane kufikisha ujumbe na kuiwezesha Tanzania kusonga mbele” Amesisitiza Bi. Fausta.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu