Thursday, October 6, 2016

WANANCHI WAHIMIZWA KUSHIRIKI KATIKA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na waandishi wa habari juu ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Oktoba 14 mwaka 2016, yatakayofanyika mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na waandishi wa habari juu ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Oktoba 14 mwaka 2016, yatakayofanyika mkoani humo.
Baadhi ya vijana wa Wilaya ya Maswa wakiwa katika zoezi la uzalishaji chaki katika kiwanda cha kutengeneza chaki kilichopo wilayani humo ambacho kinazalisha chaki zinazotambulika sokoni kama Mzinazotumika mkoani Simiyu.
Baadhi ya vijana wa Wilaya ya Meatu wakielekezwa namna ya kupima maziwa na kutambua maziwa bora yasiyo na maji, katika kiwanda chao cha uzalishaji wa maziwa yanayotambulika sokoni kama ‘MEATU MILK’
Sehemu ya Jengo la Ofisi ya Vijana wa Wilaya ya Meatu wanaojishughulisha na usindikaji wa maziwa (MEATU MILK).

Na Stella Kalinga, Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla kushiriki katika Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana mwaka 2016, yatakayofanyika mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu umepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yatakayofanyika Oktoba 14, 2016 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mtaka ameeleza kuwa Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia atashiriki Ibada ya Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere, itakayofanyika siku hiyo ya tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana, Mjini Bariadi kuanzia saa 1:00 kamili asubuhi.

Wakati huo huo Mtaka amesema maadhimisho ya wiki ya vijana yatafunguliwa rasmi tarehe 08 Oktoba, 2016 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb) katika Uwanja wa SABASABA Mjini Bariadi; ambapo shughuli mbalimbali za vikundi vya maendeleo ya vijana kutoka Halmashauri zote nchini zikiwemo za ujasiriamali pamoja na ugunduzi wa kisayansi ambao umethibitishwa na Tume ya Taifa ya Sayansi zitaoneshwa katika mabanda maalum yaliyojengwa katika uwanja huo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu