Tuesday, October 4, 2016

WASHIRIKI WA MISS TANZANIA 2016 WATEMBELEA OFISI ZA KAMPUNI YA INFOTECH INTERNATIONAL LIMITED (PII) JIJINI DAR

Mkurugenzi Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Perfect Infotech International Limited (PII), Ebenezer Msuya akizungumza na washiriki wa Miss Tanzania 2016.

“PII ni sehemu ya udhamini wa mashindano ya Miss Tanzania 2016 na kazi yetu ni kuhakikisha warembo hawa wanakuwa salama katika safari ambazo wanazifanya na hata watakapokuwa wakielekea Mwanza watakuwa wakionekana moja kwa moja usalama upo vizuri,” alisema Msuya.

Aidha Msuya alisema kuwa kampuni ya PII itaingia mkataba wa mwaka mmoja na mrembo mmoja ambaye ataonekana kuwa na vigezo vya kufanya kazi na kampuni ili waweze kufanya kazi naye kama balozi wa kampuni ya PII kwa kuitangaza na kuisaidia kukuza biashara yake.
Mkurugenzi Uendeshaji Biashara wa kampuni ya Perfect Infotech International Limited (PII), Ebenezer Msuya akizungumza na washiriki wa Miss Tanzania 2016 na waandishi wa habari.
Washiriki wa Miss Tanzania 2016.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Lino Agency ambo ndiyo waandaaji wa Miss Tanzania, Hashimu Lundenga aliishukuru PII kwa udhamini ambao wamewapatia na jambo hilo ni jipya kwao kwani waliokuwa hawajawahi kulipata na wanaamini safari yao itakuwa salama.

Mkurugenzi wa Lino Agency ambo ndiyo waandaaji wa Miss Tanzania, Hashimu LundengaMkurugenzi wa Lino Agency ambo ndiyo waandaaji wa Miss Tanzania, Hashimu Lundenga akizungumzia udhamini wa kampuni ya PII na jinsi unavyowasaidia.

“Sijawahi kutumia mfumo huo, lakini niseme kwa teknolojia ambayo wametupatia tunawashukuru, hili ni jambo zuri sana,” alisema Lundenga.
 Kiongozi wa Miss Tanzania, akiwaongoza washiriki wa Miss Tanzania 2016 kuelekea eneo la ofisi ya PII.
Meneja wa Uendeshaji Biashara wa PII, Raymond Lugina akiwaelezea jinsi wanavyofanya kazi kwa kufunga mifumo ya kiteknolojia katika magari.
Washiriki wa Miss Tanzania 2016.
Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakiwa na viongozi wa kampuni ya Perfect Infotech International Limited (PII).

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu