Wednesday, November 9, 2016

AIRTEL NA VETA YATOA ELIMU JUU YA MASOMO YA UFUNDI KUPITIA SIMU YA VSOMO

Walimu na wanafunzi wa Chuo cha VETA Kipawa wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kushoto) akifafanua juu ya ushirika kati ya Airtel na VETA kwa kuleta mafunzo ya ufundi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu yajulikanayo kama Vsomo yaani VETA Somo, katika semina iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa, Eng. Lucius Lutenganya akifafanua jambo kwa walimu na wanafunzi wa chuo hicho juu ya programu ya Vsomo yaani VETA Somo inayotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ambapo wanafunzi wa Chuo cha VETA watapata fursa ya kusoma kupitia simu za mkononi, kulia ni Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Hawa Bayumi na Mratibu wa kozi fupi na ujasiriamali VETA kipawa, Gosbert Kakiziba. Semina hiyo iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Hawa Bayumi (kulia) akielezea faida za programu ya VSOMO kwa walimu na wanafunzi wa chuo cha VETA Kipawa inayowezesha kupata mafunzo ya ufundi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu katika semina iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mratibu wa kozi fupi na ujasiriamali VETA kipawa, Gosbert Kakiziba akijibu swali juu ya kozi zipatikanazo kupitia program ya VSomo yaani VETA Somo inayowezesha kupata mafunzo ya ufundi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu, katika semina iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
Wanafunzi wa Chuo cha Veta Kipawa wakisikiliza kwa makini katika semina juu ya mpango wa VSomo yaani VETA Somo inayowezesha kupata mafunzo ya ufundi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu, ambapo wanafunzi wa VETA watapata fursa ya kusoma kwa kupitia simu za mkononi wakati wa semina iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu