Nacte yafuta leseni ya vyuo vya ufundi 26
· 20 vyasimamishiwa programu zisizosajiliwa na baraza hilo
· 2 vyasimamishwa kwa kutokuwa na usajili

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifungia vyuo vya ufundi 26 kutokana na makosa mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na kutoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kaimu Katibu mtendaji wa NACTE, Dkt.Adolf Rutayuga, alisema kuwa wamekuwa wakifuatilia vyuo vya ufundi ili kutathmini kama vinafuata viwango vya ubora wa kitaaluma vilivyowekwa na NACTE katika kutoa mafunzo. 

“Kama ilivyoelezwa katika sheria za Usajili na Kanuni za leseni, kutozingatia matakwa yoyoye yaliyowekwa na NACTE ni kosa kisheria. Kanuni zinasema kuwa hatua kali zinawezakuchukuliwa kwa kila kosa. Kulingana na matokeo ya ufuatiliaji uliofanywa na timu maalumu, Baraza lina uwezo wa kuchukua hatua dhidi ya taasisi au vyuo vinavyoshindwa kutekeleza kanuni zilizowekwa,” alisema.

Alisema kuwa baada ya kufanya utafiti wao, wamebaini vyuo 26 vilishindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na NACTE katika cheti cha usajili, huku vyuo 20 vikitoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika,wakati vyuo viwili vikiwa na vituo vya satellite/Kampasi ambavyo navyo havijathibitishwa na chombo husika.

“Baraza linaufahamisha umma kwamba limechukua hatua mbalimbali kwa vyuo vya ufundi 48 kutokana na makosa mbalimbali, yaliyofanywa na vyuo hivyo ambapo limesitisha vyeti vilivyotolewa kwa vyuo 20 ambavyo vimeshindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa kwenye Cheti cha Usajili.
“Uamuzi huu umefanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 20 ya Usajili wa Vyuo vya Ufundi ya mwaka 2001,” alisema.

Rutayuga alisema kwamba vyuo vilivyofutiwa usajili kutokana na kosa la kutoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika ni 26.“Vyuo vya ufundi vinatakiwa kupata kwa idhini ya Baraza kabla ya kuanza kutoa mafunzo yoyote. Idhini hiyo inahusu uthibitisho wa mtaala kwa ajili mafunzo yaliyokusudiwa na utambuzi wa idara iliyopangwa kutoa mafunzo hayo,” alisema. 

Juu ya vyuo vyenye vituo vya setelite, kampasi, Dkt.Adolf Rutayuga alisema kuwa Baraza linahitaji mafunzo kutolewa katika vituo vilivyosajiliwa/kampasi za vyuo vikuu baada ya kuthibitishwa kwamba vinastahili kutoa mafunzo. 

“Hata hivyo, taasisi mbili zimebainika kutoa mafunzo katika vituo vya satellite/vyuo vikuu ambavyo havijasajiliwa na Baraza na hivyo kuadhibiwa. Vyuo hivyo navyo vimefutiwa leseni,” alisema Rutayuga.

NACTE ni bodi iliyoanzishwa kisheria chini ya Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, kifungu cha 129, kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo nchini Tanzania. Chini ya sheria hiyo, ili kufikia na kudumisha hali ya mtoa mafunzo, vyuo vyote vinatakiwa viwe vimesajiliwa, vibali na kuwa mitaala iliyopitishwa na baraza. Vyuo haviruhusiwi kuanza kutoa kuanza kutoa huduma yoyote ya mafunzo bila idhini ya baraza.


1; Vyuo vya Ufundi vilivyofutiwa usajili;

Institute of Management and Development Studies – Iringa
Green Hill Institute – Mbeya
Institute of Business and Social Studies – Mbeya
Loyal College of Africa – Mbeya
Mbeya Training College – Mbeya
Mbengwenya College of Business and Information Technology –Mbinga
New Focus College – Mbeya
Shukrani International College of Business and Administration – Mbeya
Majority Teachers College – Mbeya
Rukwa College of Health Sciences – Sumbawanga
MAM Institute of Education – Mbeya
Belvedere Business and Technology College – Mwanza
Geita Medical Laboratory Sciences and Nursing Training College – Geita
Global Community College – Geita
Muleba Academy Institute – Muleba
St. Bernard Health Training Institute – Katoro, Geita
Victoria Institute of Tourism and Hotel Management – Mwanza
Gisan Institute of Health Sciences – Mwanza
Dar es Salaam Institute of Business Management – Dar es Salaam
SAMFELIS College of Business Studies – Dar es Salaam
Ellys Institute of Technology – Bunda, Mara
Tanzania Institute of Chartered Secretaries and Administrators – Arusha
Emmanuel Community College – Kibaha
Modern Commercial Institute – Dar es Salaam
Marian College of Law – Dar es Salaam


 2;Vyuo vya Ufundi vinavyotoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa;

MISO Teachers College – Mafinga 
Competence Building Network (CBN) - a Certificate in Early Childhood Education
Tusaale Teachers College - Mafinga 
Competence Building Network (CBN) - a Certificate in Early Childhood Education
The St. Joseph’s College Institute of Business and Management (SJCIBM) – Morogoro 
The Golden Training Institute – Dar es Salaam 
Nkrumah Mkoka Teachers College – Kongwa, Dodoma 
National Institute of Agriculture (Chuo cha Kilimo cha Taifa) – Arusha 
Musoma Utalii Training College – Musoma 
Mwanza Polytechnic Institute – Mwanza
Mwanza Polytechnic Institute – Maswa 
Ruter Institute of Financial Management – Mwanza 
Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Mwanza 
Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Geita 
Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Bukoba 
Singni International Training Institute – Bukoba 
Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Kahama 
Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Simiyu 
Richrise Teachers College – Geita 
Twiga Training Institute – Musoma 
Zoom Polytechnic Institute – Bukoba 
St. Thomas Training College – Shinyanga 

3: Vyuo vya Ufundi vyenye Vituo vya Satellite / Kampasi

MISO Teachers College – Mafinga
Rungemba Teachers College – Mafinga
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: