Monday, November 21, 2016

CHUO KIKUU IRINGA WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI KWA UHAKIKI WA WATUMISHI HEWA

Wahitimu Aziza Mkawa na Amina Ally wakimlisha keki mwenzao Eugenia Msahala aliyehitimu jana chuo kikuu cha Iringa
Wahitimu wa chuo kikuu cha Iringa Rubeny Nyagawa kulia ,Anna Laiza , Deodatus Mnyang'ari na Anna Lwanda wakijipongeza kwa keki baada ya kuhitimu digirii ya biashara na utawala katika chuo kikuu cha Iringa

Na MatukiodaimaBlog.

UONGOZI wa  Chuo kikuu cha Iringa (UoI) umepongeza jitihada zinazofanywa na

serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli juu ya uhakiki wa watumishi hewa wenye vyeti feki kwa madai hatua hiyo ni nzuri itasaidia kupata wataalam wenye sifa sahihi tofauti na ilivyokuwa awali kuwa na utitiri wa watumishi wasio na uwezo.

Pongezi hizo zimetolewa jana wakati wa mahafali ya chuo hicho na mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, askafu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dkt. Odenburg Mdegela alisema kuwa zoezi hilo linapembua mchele na chuya na kuwaacha wale wenye vyeti halai tu.

Alisema ilikuwa si sahihi mmoja akae darasani miaka mitatu na mwingine apate cheti kutoka kariakoo tena kikiwa a ufaulu wa juu kuliko Yule aliyekaa darasani.

Dkt. Mdegela alisema watu hawa wanapokutana kazini Yule alipata vyeti bandia vyenye ufaulu wa hali ya juu anakuwa hajui kazi jambo lililokuwa likirudisha nyuma maendeleo ya taasisi nyingi na nchi kwa ujumla.

“Uhakiki wa vyeti unapaswa kuungwa mkono na wadau wote wakiwemo wa elimu kwa kuwa hali ilikuwa mbaya huku wale wenye vyeti badia vikiwa na ufaulu wa hali ya juu ilhali hawajui kazi”, alisema Dkt. Mdegela

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu