Meneja masoko wa Kituo cha televisheni cha EATV, Roy Mbowe akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, wakati wa kutangaza makundi mapya matatu yatakayoshindaniwa katika tuzo za Eatv (EatvAwards) zinazotaraji kufanyika Desemba 10 mwaka huu. Wanne kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA), Godfrey Mwingereza.
---
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

KITUO cha televisheni cha Eatv leo kimetangaza makundi mapya matatu yatakayoshindaniwa katika tuzo za Eatv Awards zinazotaraji kufanyika Desemba 10 mwaka huu.

Makundi hayo ambayo yametangazwa leo mapema jijini Dar es Salaam na Meneja masoko wa kampuni hiyo Roy Mbowe katika mkutano wa waandishi wa habari na waandaaji wa tuzo hiyo katika hoteli ya Sleepway .

“tuzo hizi zenye vipenfgele 10 ambazo dhamira yake ni kuwatunza wanamuziki na wasanii wa filamu zilianza kwa kuwaomba wasanii wajipendekeze wenyewe kwa kujaza fomu maalum za kuwania tuzo ambapo wanaotajwa leo ndio waliofuta utaratibu kupitia mchujo wa awali”amesema Roy.

Amesema kuwa makundi yaliyotanjwa leo ni wimbo bora wa mwaka ambapo wanaoshindania ni , John Makini na wimbo wa Don’t Bother, Lady Jaydee na wimbo wake wa Ndindindi, Navy Kenzo na wimbo wa wao wa kamatia chini, Ali Kiba na wimbo wake wa Aje na Ben Paul ambae ameingia na wimbo wa Moyo Mashine.

Kundi la pili ni mwanamuziki bora wa kiume ambapo wanaoshindania George Sixtius (G-nako) na wimbo wa Arosto, Nurdin Billal(Shettah) na wimbo wa Namjua, Beanard Paul(Ben Paul) na wimbo wa Moyo Mashine, Hamis Mwijuma (Mwana Fa) na wimbo wa asanteni kwa kuja na wa mwisho ni Ally Kiba na wimbo wake wa Aje.

Alimaliza kwa kutaja kundi la mwisho litakalo shindaniwa kuwa ni mwanamuziki bora wa kike ambapo wanaotajwa kuwania tuzo hiyo ni Lilian Mbabazi na wimbo wa Yoola,Ruby na wimbo wa Forever sijuti, Linah Sanga na wimbo wa No Stress, Vannesa Mdee na wimbo wa Never Ever na lady Jaydee na wimbo wake wa Ndindindi.

Kwa upande wake katibu mkuu wa baraza la sanaa nchini Tanzania (BASATA), Godfrey Mwingereza, amesema kuwa tuzo hizo zimefata vigezo vyote kwa kuwa wasanii wote ambao wameshiriki katika tuzo hizo wamesajiliwa na basata hivyo wale wote waliojipendekeza lakini awakusajiliwa walikuwa wanajiondoa wenyewe kwenye mashindano kwa kukosa sifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: