Thursday, November 17, 2016

KARATE NI TAALUMA NDIYO MAANA KUNAMAFUNZO KILA MWAKA : SENSEI KALONGA

Rais wa Shirikisho la Karate nchini Tanzania ambaye pia ni mwenyekitti wa chama cha Karate mkoani Kilimanjaro Sensei Geofrey Kalaonga.
Hamza Mzonge ambaye ni kaimu mwenyekiti wa chama cha karate mkoa wa Kilimanjaro
Sensei Hamis Wembo Katibu mkuu mtendaji wa chama cha karate mkoa wa Kilimanjaro pia ni mkufunzi wa jeshi la polisi mkoani hapo.
Sensei Ibrahim Mganga ambayaye ni mkufunzi wa chuo cha polisi Moshi (C CP)

Na Woinde Shizza, Kilimanjaro

Tamasha la kutunukiwa vyeti kwa wachezaji waliofuzu madaraja ya mikanda tofautitofauti limefanyika hivi karibuni katika manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.

Tamasha hilo limeandaliwa na chama cha karate mkoa wa Kilimanjaro huku ambapo zaidi ya vijana 54 wa kike 5 na wakiume 49 walishiriki katika mchezo huo,ambapo umeshirikisha vilabu viwili tofauti ambavyo ni Mo town club na Suparampe zote zinatoka manispaa ya Moshi mjini.

Raisi wa Shirikisho la karate nchini Tanzania na mwenyekiti wa chama cha karate mkoani Kilimanjaro Sensei Kalonga amesema kuwa vijana hao wamepata mafunzo kwa mwaka mmoja na niutaratibu wa chama cha karate.

Kalonga amesema kuwa wameandika historia mpya kwa kuupigania mchezo wa karate mkoa wa kilimanjaro na Tanzania nzima,pia umuhimu wa maendeleo ya vijana kupitia mchezo wa Karate,amesema mchezo huo ni taaluma ndiyo maana wamekaa darasani na kufuzu.
Club mbili za Karate wakiwa katika maonyesho ya pamoja katika tamasha lilifanyika katika shule ya msingi mwenge iliyopo Manispaa ya Moshi mjini, ambazo ni Mo town Club na suparampe club zpte za Moshi mjini.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wahitimu wa mafuzo ya karate wakionyesha yale waliyojifinza kabla ya kukabiddiwa vyeti vyao hapo pia wakina dada wamo ndani wakionyesha kata mbalimbali.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mwanadada Matilda Mallya akifanya yake katika karate kwenye tamasha hilo la kukabidhiwa vyeti kwa wahitimu lililofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Mwenge iliyopo Manispaa ya Moshi mjini ambapo yeye alipewa cheti kwa kufuzu mafunzo ya mkanda wa brown.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Krate akipokea cheti chake katika tamasha lililofanyika katika shulke ya msingi mwenge iliyopo manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro .

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu