Ukisoma kwenye Hosea 6:6a utaona anasema nataka FADHILI na si sadaka, neno Fadhili kwenye tafsiri ya biblia ya THE MESSAGE utaona neno linasema "I am after LOVE that last's" kumbe FADHILI Mungu anayo itafuta ni UPENDO usio koma kwa Mungu, ukiendelea mbele utaona anasema "and No more religion" kumbe wengi tunaweza tukawa tunatoa sadaka lakini ni kidini na si kwa maelekezo ya Roho Mtakatifu.

Mara ya mwisho tulijifunza kuwa hakuna kitu Mungu anakipenda kama kumtolea sadaka/dhabihu kwa upendo kutoka ndani ya moyo wako. Wakristo wengi tumetengenezewa mazingira ya udini mwingi na kuliko kumsikiliza Roho wa Mungu. Ukweli wa hili ni hii, ni raha sana kutembea katika maelekezo ya Roho wa Mungu maanaa anasema waongozwao na Roho ndio wana wa Mungu, the proof of sonship sio kutoa mamilioni ya pesa kama sadaka ila hiyo uliyo toa ni maelekezo ya Mungu? Na ulipo peleka ni mahali Mungu anataka? Na kama ndio hapo imeenda kwa wakati sahihi?? Huo ndio uwana wa Mungu tunai zungumzia.

Sadaka/dhabihu unayo itoa Mungu anaangallia Upendo/Fadhili ndani ya Moyo wa mtoaji hiyo sadaka. Unapo mpa mtu sadaka ndani ya moyo wako una nini kimeujaza moyo wako?? Giving is a dangerous act, if you act without Spirit of God, but also is a privilege before God to give. Ni hatari sana kutoa kama hamna upendo ndani yako, maana unaweza kupokea Laana badala ya baraka.
#LOVETHATLAST
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: