Tuesday, November 15, 2016

MAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU HASSAN AKWEA AIR TANZANIA KUELEKEA JIJINI MWANZA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa tiketi ya kusafiria ya Shirika la Ndege la Air Tanzania, kutoka kwa Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Professa Makame Mbarawa, kabla ya kusafiri na Ndege hiyo kuelekea Jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi, leo Novemba 14, 2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na marubani na wahudumu wa ndege mpya aina ya Bombardeir Q 400 baada ya kukabidhiwa ticket ya kusafiria na Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Professa Makame Mbarawa kulia leo Novemba 14, 2016 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ambapo Makamu wa Rais alisafiri na ndege hiyo kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na vyombo vya habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipungia wakati akiindia ndani ya Ndege ya Air Tanzania aina ya Bombardeir Q 400.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya Abiria waliokuwemo ndani ya Ndege hiyo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu