Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwa anapanda kwenye gari ya polisi mara baada ya kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na kuwekewa na pinganizi la dhamana.
Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwa anapanda kwenye gari ya polisi mara baada ya kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na kuwekewa na pinganizi la dhamana.
Mke wa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Neema Lema akiwa anaondoka mahakamani kumsindikiza mme wake mara baada ya mahakama kuisha na lema kuamriwa kwenda mahabusu ya magereza hadi ijumaa ambapo kesi yake itatajwa tena

Na Woinde Shizza, Arusha.

Vilio na majonzi vimetawala katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha Mara baada ya Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na kuwekewa na pinganizi la dhamana.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mabishano ya kisheria kuhusiana na dhamana ambapo mawakili wa serikali wakiongozwa na wakili Matenus Marandu pamoja na Paulo Kadushi kupinga dhamana ya Mbunge huyo kutoka na kile mawakili wa serikali walichodai kuwa iwapo atapewa dhamana ataenda kuendelea kufanya mikutano ya adhara ya uchochezi.

Aidha hoja zingine zikizotajwa na mawakili hao walieleza mahakama hiyo mbele ya hakimu mkazi Desderi Kamugisha kuwa uchunguzi wa kesi zingine  za uchochezi zinazomkabili Mbunge huyo zinaonyesha alipewa dhamana ili ajirekebishe lakini ajirekebishi na amekuwa akirudia rudia makosa
yanayofanana kila Mara.

Kwa upande wake jopo la mawakili wasomi wa upande wa mshitakiwa wakiongozwa na John Malya , Sheck Mfinanga ,Ahmed Hamis na Charles Adiel Mshitakiwa ana Haki ya kupata dhamani ukizingatia kesi inayomkabili bado uchunguzi wake haujakamilika hivyo anahaki ya kupewa dhamana kulingana na sheria na katiba inavyo dai aidha waliongeza kuwa mtuhumiwa ni Mbunge wa bunge la Tanzania hivyo mahakama inawajibu wa kumpatia dhamana kwaajili ya kuendelea na majukumu ya wananachi ambao wamemchagua.

Waliongeza kuwa pamoja na Mbunge huyo kukabiliwa na kesi mbili ambapo alitaja kesi ya kwanza inayomkabili ni namba 440 na ya Pili ninamba 441 za mwaka 2016 ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya muheshiwa Rais ambapo alisema maneno kuwa nchi hii aita tawalika na itaingia kwenye machafuko iwapo Rais atafuata katiba na sheria hivyo bado anaamini makosa hayo yanastaili kupata dhamana kama sheria ya makosa ya mwenendo ya jinai.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili hakimu kamugisha alihairisha shauri hilo adi November 11 itakapo kuja kutajwa tena na kutolewa uwamuzi mdogo iwapo mshtakiwa Lema atapata dhamana au Ataendelea kukaa kizuizini .

Wakati Mbunge huyo akiondoshwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi Lema alionekana kujiamini huku akiwa ameshika biblia takatifu  ndipo wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema waliangua vilio na mayowe huku wakilia Mbunge huyo.

Akitoa tamko Mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha Amani Golugwa aliwaomba wananchi wa Mkoa wa Arusha kuwa wavumilivu katika kipindi hichi kigumu cha Mbunge wao kushikiliwa na kuwataka kujitokeza kwa wingi mahakamani kufatilia mwenendo wa kesi ya Mbunge wao.

Awali kabla ya kuanza kusikiliza kesi hiyo jaji Salma Majimbi alimuamuru mwanasheria wa serikali kumleta mshitakiwa Lema ndani ya nusu saa mahakamani hapo ,baada ya kukaa mahabusu ya polisi ndani ya masaa 175 kinyume cha she ria ya makosa ya jinai.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: