Friday, November 11, 2016

MBUNGE WA DIMANI, HAFIDH ALLY TAHIR AFARIKI DUNIA MJINI DODOMA

Tumeondokewa na Baba Yetu, Babu Yetu, Kaka Yetu, Mwenzetu, Kiongozi Wetu Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir - Mbunge wa Uvccm Jimbo la Segerea Dimani Zanzibar. Mheshimiwa Hafidh Ally ni kiongozi mwenye mvuto na ukaribu mno na wananchi. Ni mwanamichezo na mwanakandanda kindakindaki, alikuwa miongoni mwa Marefa wa mwanzo ws FIFA barani Afrika ambapo amechezesha mechi nyingi sana za soka za kimataifa. Mheshimiwa Hafidh Ally pia alikuwa mtangazaji wa iliyokuwa Redio Tanzania ambapo miongoni mwa manguli aliyofanya nayo kazi ni Marehemu David Wakati "Magunia". Katika utawala wa Rais wa Tano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ); Mheshimiwa Hafidh Ally alikuwa Msemaji Mkuu wa Serikali. Aidha Mheshimiwa Hafidh Ally ashawahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Rahaleo.

Mheshimiwa Hafidh Ally alikuwa ni mwanasoka hadi dakika ya mwisho kwani alichezea timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Yanga iliyoinyuka ile timu shindani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Simba, ambapo alifunga magoli matatu katika mechi hiyo. Hivi jana, Mheshimiwa Hafidh Ally amechaguliwa kuwa Katibu wa Timu hiyo ya Bunge, chini ya Uenyekiti wa Mbunge wa Kilolo Mheshimiwa Mwamoto.

Mchango wake Mkubwa utakumbukwa daima na sote tunaungana na familia yake, wananchi wa jimbo la Dimani chini ya Mwakilishi Mheshimiwa MwinyiHaji Makame Mwadini, Wazanzibari wote chini ya Kiongozi wetu Dkt Ali Mohamed Shein - Rais Wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na pia Watanzania wote chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli. Tunatuma salamu za rambirambi maalum kwa Waheshimiwa Wabunge wote na Watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi Mahiri wa Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) - Spika wa Bunge.

Tunamuombea duwa kwa Mola amghufirie na kumrehemu

Inalillahi wainailaihi rajiun
A. H. Makame and Family.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu