Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza wakati alipotembelea kituo kipya cha kupooza na kusambaza umeme cha City Centre jijini Dares Salaam, Novemba 5, 2016. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Shirika hilo kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende Mgaya.
Mhandisi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha Kupoozea na kusambaza umeme cha Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, ametembelea vituo vitatu vipya vya kupooza na kusambaza umeme vilivyo kwenye mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam leo Novemba 5, 2016.

Vituo alivyotembelea ni pamoja na kile cha katikati yajiji, (City Centre), kilicho jirani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kituo cha Kurasini na kituo cha Ilala Mchikichini.

Kwa takriban mwezi mmoja sasa, TANESCO kwa kushirikiana na wahandisi kutoka kampuni za Kijapani, Yachiyo Engineering Co Limited, Sumitomo, Takaoka na National Construction Limited, wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kubadilisha laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora wa hali ya juu.
Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona akielezea hatuailiyofikiwa hadi sasa ya uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam
Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, akielezea teknolojia ya kisasa ya mashine ndogo yenye kufanya kazi kubwa
Kituo cha City Centre
Mhandisi Mramba, akitembelea mitamboya kituo cha City Centre.
Fundi mitambo ya umeme akiwa kazini kituo cha Ilala Mchikichini
Mhandisi Mramba, (kushoto), akizungumza wakati alipotembelea kituo cha Kupooza na kusambaza umeme cha Kurasini kujionea maendeleo yaujenzi wa kituo hicho.
Mitambo ya kituo cha kupoozea na kusambaza umeme cha Kurasini
Mhandisi Chegere (wapili kulia), akipatiwa maelezo ya mitambo ya kituo cha City Centre
Jengojipya la kituo cha Ilala Mchikichini.
Moja ya mashine mpya kituo cha Ilala Mchikichini.
Chumba cha mitambo mipya ya umeme kituo cha Ilala Mchikichini.
Mhandisi Mramba, akiwa na wahandisiwenzake, Chegere (kulia) na Mgaya, kwenye kituo cha City Centre.
Mitambomipya kituo cha Kurasini
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: