Masoko ya Tanzania yamekuwa yakikumbana Na changamoto nyingi kutokana Na hali ya kiuchumi inayoendelea nchini. 
 
Tanzania inaonekana kuwa miongoni mwa nchi zinazokua imara katika masoko kati ya baadhi ya nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara. 
 
Pia jiji la Dar es Salaam limekuwa miongoni mwa miji inayokua kwa haraka ikiwa na idadi kubwa ya watu. Kutokana na ukuaji wa uchumi Tanzania, kumekuwa na ongezeko la ushindani kwa wafanya biashara wa maduka ya rejareja, hasa Dar es salaam, jiji linalochukuliwa kama kitovu cha uchumi wa nchi. Huku mitaani yapo maduka yanayouza bidhaa za rejareja na zenye ubora tofauti tofauti.

Katika kukabiliana na ushindani huo, Mlimani city wameamua kuja na Mlimani City wikiendi Bonanza kuanzia tarehe 12 na 13 mwezi huu, ikiwa ni moja ya hatua iliyofanyika na mlimani city mall, katika kuhakikisha ongezeko la masoko na biashara kwa ujumla.

Akiongelea kampeni hiyo Mkurugenzi mkuu wa mlimani City bwana Pastory Mrosso amesema kuwa Kila duka liliopo mlimani city litakua likitambulisha ofa kabambe katika siku hizo mbili ili wateja wao waweze kuanza msimu wa sikukuu kwa mafanikio.

Kwa msimu huu wa sikukuu unaokuja, wafanya biashara wanatumia njia tofauti kuwavutia wateja katika maduka yao. Tanzania ina namba kubwa ya makampuni ya kimataifa yaliyowekeza kibiashara hapa Dar es salaam. Supamaketi kubwa , Game, kutoka Afrika kusini na Nakumatt kutoka Kenya wana idara za bidhaa lukuki pale Mlimani city- mall kubwa zaidi hapa Tanzania. Mlimani city inakuletea “wikiendi Bonanza” yenye nia ya kuongeza wateja zaidi kwa kupitia ofa mbalimbali kutoka katika maduka yao.

Kampeni hii inayoongozwa na Mlimani city mall, wikiendi hii ya tarehe 12 na 13 Novemba kwa kushirikiana na maduka yote katika kukuletea ofa za nguvu ili kuchochea biashara katika wikiendi hii. Ofa hii inagusa bidhaa nyingi mbalimbali kama nguo, vitu vya nyumbani, fasheni, mabenki na bidhaa nyingi tofauti katika maduka mlimani city.

Mlimani city ni mall kubwa zaidi Tanzania yenye mita za mraba 19,000. Ni mall kubwa ya kwanza kwa Dar es salaam kuwa na kiyoyozi cha kuaminika. Uwepo wa bidhaa za kimataifa kutoka Afrika Kusini na Kenya kunaifanya mlimani city kuwa kituo maarufu kwa wazawa na watalii wote Dar es salaam. Inakupa eneo kubwa la maegesho ya magari lenye uwezo wa kupokea wastani wa magari 835 na kulindwa kwa usalama wa hali ya juu muda wote. Mall hii ni uwanja wa frame 54 ambazo zinahusishwa migahawa, maduka ya nguo, fenicha, mahitaji ya nyumbani, maduka ya simu n.k. pia ina supamaketi kubwa Tanzania kutoka nchi za nje; Game na Nakumatt. Pia maduka ya nguo ya kimataifa kama Splash, The Baby store, Mr. Price. Pia wateja hawatakiwi kuhofi kuhusu mihamala yao maana huduma za kibenki nazo zipo kupitia matawi ya NMB, CRDB, Exim Bank na NBC. Yeyote anaweza kusema sasa soko limeandaliwa vyema, na kwa kutumia mikakati imara kwa ajili ya kuhakikisha ubora na kufikia matarajio mapya kibiashara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: