Naibu mthibiti mkuu ubora wa shule kanda ya nyanda za juu kusini Aldo Masonda Bw Aldo Masonda
Na MatukiodaimaBlog

KUFUATIWA uwepo wa utitiri wa shule binafsi za awali na msingi za English Midium au
kiswahili Midium School maeneo mbali mbali mkoani Iringa wazazi mkoani hapa waonywa kuacha kuwaandikisha watoto wao katika shule hizo bubu zisizosajiliwa ili kuepuka kuchukuliwa hatua mzazi na mmiliki wa shule husika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jana naibu mthibiti mkuu ubora wa shule kanda ya nyanda za juu kusini Aldo Masonda alisema kuwa mzazi kabla ya kumpeleka mtoto wake kuanza elimu ya awali ama ya msingi kwenye shule yoyote ni lazima kuomba kupatiwa namba ya usajili wa shule husika kabla ya kumwandikisha mtoto na iwapo atakuwa na hofu na namba ya usajili wa shule husika afike ofisi za mratibu elimu kata ama ofisi za elimu wilaya na mkoa kuweza kupata uhakika wa usajili wa shule husika.

Hivyo alisema ni kosa kwa mzazi kumpeleka mtoto shule isiyo sajiliwa na kuepuka kuwajibishwa mzazi na mmiliki wa shule hiyo ni vizuri wazazi kufika ofisi za elimu kujiridhisha ama kufika ofisi ya mthibiti ubora wa shule ngazi ya wilaya au ofisi ya kanda na kwa wale wanaoweza kuingia katika tovuti ya wizara ya elimu ambako wataona shule zote nchi nzima ambazo zimesajiliwa na zina sifa ya kuitwa shule.

Alisema kumezuka tabia ya watu kuendesha shule pasipo kuwa na usajili jambo ambalo ni kosa la kisheria na iwapo itabainika mhusika atachukuliwa hatua na kuwa tayari katibu mkuu wa wizara amekuwa akichukua hatua mbali mbali ya kuwaandikia barua wale wote wanaoendesha vituo vya elimu wanavyoviita ni shule za English Midium.

Masonda aliwataka wananchi wote kuendelea kutoa taarifa katika ofisi yake iwapo watabaini kuwepo kwa shule bubu katika maeneo yao kwani kwa kimsingi ni marufuku kwa mtu yeyote kutoa elimu kuanzia watoto saba na kuendelea kwa kuwa iwapo itabainika kuwa mtu anatoa elimu kwa watoto kuanzia saba na kuendelea bila kuwa na namba ya usajili ni kosa.

Alitaja sifa ya kuitwa shule ni pamoja na kuwa na vyumba vya madarasa vizivyopungua saba ,vyoo matundu yasiyopungua 10 ,ofisi za walimu tatu pia kuwa na ardhi yenye ukubwa kuanzia heka tatu ila alisema wapo baadhi ya watu wamekuwa wakivunja sheria kwa kuanzisha shule bila ya kuzingatia taratibu.

Kuhusu mambo kumi muhimu ya kuzingatia katika usajili wa shule alisema ni pamoja na andiko la mradi ,hati miliki ya kiwanja ,kibali cha kujenga shule ,site plan ya shule , barua ya uthibitisho wa kuwa mwenye shule ,barua ya uthibitisho kuwa meneja wa shule, taarifa ya mhandisi wa majengo wilaya,taarifa ya bwana afya wilaya, taarifa ya ukaguzi wa mwisho wa shule, orodha ya majira ya walimu na vyeti
vyao, mikataba ya ajira ya wafanyakazi na fomu ya usajili wa shule (form no RS 8).

Hivyo alisema iwapo kuna shule imeanzishwa na inapokea wanafunzi pasipo kufuata taratibu hizo kumi katika uanzishwaji wake mmiliki wa shule hiyo atakuwa amevunja sheria na ikibainika atawajibishwa kisheria japo aliwataka wananchi kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kujenga shule ila kwa kufuata taratibu zote.

Masonda alisema wao wanasimamia ubora wa shule zote kuanzia shule za awali hadi vyuo vya ualimu vya binafsi na serikali na kuwa changamoto kubwa wamekuwa wakiipata kwa taasisi binafsi kwa baadhi
ya watu kuanzisha kuanzisha shule bubu.

Kutokana na uchunguzi uliofanywa na mtandao wa matukiodaimaBlog katika mkoa wa Iringa kumekuwepo kwa shule zinazoendeshwa pasipo kusajiliwa huku wazazi wakitozwa mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kulipia ada.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: