Friday, November 25, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMFUNGULIA NJIA MHE. MAKONDA KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA YA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kwa juhudi anazofanya katika ziara yake kwa kusikiliza kero za Wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Rais Dkt. Magufuli ambaye alimpigia mkuu huyo wa mkoa wakati alipokuwa akisikiliza kero za Wananchi katika Kata ya Mbezi Luis eneo la Malamba Mawili ambako aliweza kumsisitiza kuwa aendelee kutumbua watu huko huko aliko.

“Endelea hivyo kutembelea wananchi na kutoa ufafanuzi kwa sababu nyingine ufafanuzi huu kama ungetolewa mapema wala wananchi wasingekuwa na sababu ya kuja kuuliza maswali kwa hiyo endeleeni hivyo hivyo na juhudi za Dar es Salaam na wakuu wa Wilaya yako na watendaji wote kwa kazi nzuri mnazozifanya kwa kusikiliza kero zao bila kujali vyama vyao bila kujali makabila yao na uendelee kutumbua huko huko” amesema Rais Magufuli.

Amemtaka pia kuendelea kupiga kazi na kumwabia kuwa yeye yupo nyuma yake kwani amevunja mwiko wa viongozi waliokuwa wanapendelea kukaa ndani.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu