Sunday, November 6, 2016

RC IRINGA AMPONGEZA SALIM ABRI ASAS KUSAIDIA KUOKOA MAISHA YA MAJERUHI WA AJALI

Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas (kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwausalama kwa mkoa wa Iringa leo , mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza zawadi maalum ya kamati ya usalama barabarani mkoa kutokana na mchango wake mkubwa kwa kamati hiyo
Kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Iringa wakijiandaa kutoa elimu katika viwanja vya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani.
Baadhi ya wananchi na watu wenye ulemavu wakiwa katika viwanja vya maadhimisho hayo
Mwakilishi wa wakala wa barabara mkoa wa Iringa akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Iringa na watu mbali mbali waliotembelea banda hilo kuona shughuli zinazofanywa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza akitoa hotuba yake leo wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani, kulia kwake ni mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas na katibu wake RTO Leopold Fungu wakifuatilia hotuba hiyo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza akihamasisha upimaji afya na uchangiaji damu katika banda la HOspitali ya Rufaa mkoa wa Iringa ambao walishiriki maadhimisho hayo ya wiki ya nenda kwa usalama mkoa wa Iringa leo kwenye viwanja vya stendi kuu ya mkoa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza (wa tatu kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau na kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo katika viwanja vya Stendi kuu , kushoto kwake ni katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu ,Kaimu RPC , DC Iringa Richard Kasesela ,Naibu meya wa Manispaa ya Iringa Mh. Lyata na kutoka kushoto wa kwanza ni katibu wa kamati ya usalama barabarani mkoa Leopold Fungu na mwenyekiti wake wa kamati Salim Abri Asas.
Dc Iringa Richard Kasesela akipata maelezo katika banda la zima moto.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza akiwa akishirikiana na mwanafunzi wenye ulemavu wa ngozi toka Lugalo sekondari Semeny Sadick kuzima moto uliowashwa na kikosi cha zimamoto na uokoaji ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya uzimaji moto baada ya kikosi hicho kutoa elimu katika shule zote za Manispaa ya Iringa.
Wasanii toka Mkwawa Magic Site Iringa wakionyesha ujuzi wa kucheza na nyoka aina ya chatu

Na MatukiodaimaBlog

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ameipongeza kazi kubwa inayofanywa na kamati ya usalama barabara mkoa wa Iringa chini ya mwenyekiti wa kamati hiyo Salim Abri Asas ambae amekuwa ni msaada mkubwa katika kuokoa maisha ya watanzania wanaopata ajali ndani ya mkoa kwa kujitolea misaada mbali mbali ikiwemo ya dawa na usafiri.

Akitoa pongezi hizo leo wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama ambayo imeadhimishwa kimkoa katika viwanja vya stendi ya mabasi yaendayo mikoani mjini Iringa ,mkuu huyo wa mkoa alisema mbali ya kuwepo kwa wadau mbali mbali katika kupunguza ajali na kusaidia pindi ajali zinapotokea ila serikali yake ngazi ya mkoa inatambua mchango mkubwa unaotolewa na familia ya mfanyabiashara Asas katika kusaidia kuokoa roho za watanzania pindi wanapopatwa ajali.

“Kana mambo mengi makubwa ambayo Asas amekuwa akijitolea kuyafanya kwa ajili ya kunusuru maisha ya majeruhi wanaopatwa na ajali ndani yA mkoa wetu mfano katika ajali iliyotokea Changalawe Mafinga kwa kuhusisha basi la Majinja ajali iliyoua watu zaidi ya 50 na kujeruhi wengine wengi …msaada mkubwa wa kuokoa roho za majeruhi kwa kujitolea dawa zilionyeshwa na Asas ….mimi nikiwa ni mkuu wa mkoa na serikali ya mkoa tunapongeza kazi nzuri ya Asas na familia yake katika kuwaidia kuokoa roho za majeruhi naomba Mwenyezi Mungu azidi kumuongezea pale anapopunguza kwa ajili ya wengine”

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu