Monday, November 7, 2016

SERIKALI YA CHINA YAKUBALIANA NA SERIKALI YA TANZANIA KUJENGA NYUMBA ZA MAKAZI YA MADAKTARI NA WATALAAM WA AFYA

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imekubaliana na Serikali ya Tanzania kujenga nyumba za makazi na ofisi kwa ajili ya madaktari na watalaam wengine wa afya kutoka china itakayogharimu pesa za kitanzania bilioni 10.

Makubaliana hayo yamefikiwa leo kwa utiaji wa saini kati ya nchi hizo mbili.

Ujenzi huo utafanyika kwenye eneo lililopo Oysterbay jijini Dar es salaam.

Katika utiaji sahihi ya makubaliano Tanzania iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya na kwa upande China uliwakilishwaa na mwakilishi wake Mkuu Lin Zhiyong.
Katibu Mkuu wizara ya afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya kulia na Mwakilishi Mkuu wa madktari wa China Lin Zhiyong wakisaini makubaliano hayo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu