Sunday, November 27, 2016

UBA YATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WA MAHITAJI MAALUM PUGU SEKONDARI

Wanafunzi wa Pugu sekondari wakishusha kwenye gari vifaa vilivyokabidhiwa nabenki ya UBA kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum
Mkurugenzi mkuu wa Benki ya UBA, Peter Makao akiwa meneja operesheni Omary wakikabidhi mafuta ya ngozi kwa kijana mwenye ulemavu wa ngozi, Daudi Nyangusi na Meneja ufadhili wa eleimu kutoka TEA , Tito Mganwa.
Mkurugenzi mkuu wa Benki ya UBA, Peter Makao akiwa meneja operesheni Omary wakikabidhi vitabu kwa wanafunzi Salum Mohamed na Ramadhani Juma pamoja na Meneja ufadhili wa elimu kutoka TEA, Tito Mganwa.
Wafanyakazi waUnited Bank of Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wenye ulemavu wa shule ya Sekondari ya wavulana Pugu jijini Dar es Salaam

Afisa masoko wa UBA , Evance Chandarua akimkabidhi begi, Ramadahani Juma
---
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Benki ya United Banko of Africa(UBA), leo imetoa viti Magodoro, Viti,Magongo ya kutembelea na vitabu vya kujisomea kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya shule ya sekondari ya wavulana Pugu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kutoa vifaa hivyo Meneja wa benki hiyo nchini, Peter Makao, amesema kuwa wamechagua kutoa vifaa hivyo katika shule hiyo kutokana na mahitaji ya watoto hao ambao wamekuwa wakisoma katika mazingira magumu.

“Vitu hivi ambavyo tumevitoa leo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia watoto hawa wenye mahitaji maalum kusoma kwa mawazo kwa kujiona kwamba wao ni sehemu hii ya shule kwa kupata mahitaji yao wote kama ilivyo kwa wengine”Amesema Makao

Ametoa wito kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii hili waweze kufanikiwa katika jamii na baada wajivunie kuwa walisoma Pugu.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu