Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akizungumza wakati wa mkutano na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki waliotembelea idara hiyo, ikiwa ni ziara yao ya kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na idara hiyo ikiwemo suala la pasi za kusafiria katika nchi hizo.Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Abubakari Akida)
Kaimu Kamishna Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishna Abbas Irovya, akizungumza wakati wa mkutano na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki waliotembelea idara ya Uhamiaji kujadili shughuli zinazofanywa na idara hiyo, ikiwa ni ziara yao ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na nchi za Afrika Mashariki ikiwemo suala la pasi za kusafiria katika nchi hizo.Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.( Picha na Abubakari Akida)
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Tawi la Tanzania baada ya kutembelea Makao Makuu ya Idara hiyo katika kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na idara .Watatu kulia ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Makongoro Nyerere.Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Abubakari Akida).
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji akizungumza wakati wa mkutano na Wakuu wa Idara ya Uhamiaji(hawapo pichani).Wabunge hao walitembelea idara hiyo kujifunza shughuli zinazofanywa na idara .Kulia ni Mbunge Makongoro Nyerere na Kushoto ni Angela Kizigha.Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam.( Picha na Abubakari Akida)
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi akizungumza wakati wa mkutano na Wakuu wa Idara ya Uhamiaji(hawapo pichani).Wabunge hao walitembelea idara hiyo kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa ikiwemo utoaji wa pasi za kusafiria katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kushoto ni Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki Twaha Taslima. Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Abubakari Akida)
KMwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Tawi la Tanzania, Makongoro Nyerere(kulia) akizungumza wakati wa mkutano na Wakuu wa Idara ya Uhamiaji(hawapo pichani).Wabunge hao walitembelea idara hiyo kujifunza shughuli zinazofanywa na idara hiyo . Wengine ni Wabunge Shyrose Bhanji(kulia) na Angela Kizigha(kushoto). Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam.( Picha na Abubakari Akida).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: