Monday, November 21, 2016

WANANCHI WA MBAGALA - KIBURUGWA WAJADILI MAAGIZO YA RPC MUROTO KUHUSU ULINZI NA USALAMA

Kijana wa Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, akizungumza kwenye mkutano wa wakazi wa mtaa huo kujadili maagizo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Muroto kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama kwenye ngazi ya Mtaa. Mkutano huo umefanyika Novemba 20, 2016
Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, Bw.Kassim Mohammed Mnyoge, akizungumzia maagizo hayo.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID.

WAKAZI wa Mtaa wa Mbagala- Kiburugwa, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wamefanya kikao Jumapili Novemba 20, 2016, cha kujadili maagizo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Muroto kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama ngazi ya Mtaa.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata Bw.Saleh Kaitani, alisema, kikao hicho kitajadili mambo mawili, mosi ni maagizo ya SACP Muroto na pili ni masuala ya mpango wa kusaidia kaya masikini wa TASAF.

Kusuhusu suala la ulinzi na usalama, Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa huo, Bw. Kassim Mohammed Mnyoge alisema, SACP Muroto katika kikao chake na watendaji kilichofanyika Oktoba 28, 2016 kwenye shule ya msingi Kigungi, alitoa maagizo kadhaa kuhusu hatua za kuchukua katika kuhakikisha wananchi wanashirikishwa katika suala la ulinzi na usala.

“Kila mjumbe wa mtaa kwa kushirikiana na Mratibu, waorodheshe katika daftari wakazi wa mtaa husika ili kujua idadi yao na shughuli wanazofanya.” Alisema Bw. Kassim wakati akiwasilisha taarifa kwa wananchi.

Mtaa wa Kiburugwa una wakazi wanaofikia 18,000 kwa mujibu wa Bw. Kassim.

Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo la Ulinzi na Usalama, Bw. Kassim alisema, SACP Muroto ameagiza wananchi mjadili jinsi ya kushiriki katuika suala la ulinzi na usalama kwenye mitaa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu