Polisi wa kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es Salaam, akiongoza bajaj wakati wa maandaano ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoa wa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga Novemba 7, 2016. Katika uzinduzi huo ambao mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bw. Felix Lyavivaakimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Kikosicha usalama barabarani kilitumia wasaa huo kuwaelimisha wananchi, sheria mbalimbali zinazosimamia usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari kwa madereva wa vyombo vya moto, na matumizi ya alama za kuongoza magari pamoja. Wilaya zote tatu na zile mpya ziliwakilishwa na makamanda wa vikosivya usalama barabarani, wakiongozwa na wajumbe wa baraza lausalama barabarani la mkoa. Sambamba na hayo, palikuwepona burudani mbalimbali, wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Tunda Man na Msaga Sumu ambaye wimbo wake unatumika kutangaza hatua za kuzngatia katika kuzingatia sheria za usalama barabarani, lakini pia walikuwepo wasanii wa jeshi la polisi na wale wanafunzi ktoka shule ya Jeshi la Wokovu. Uzinduzi huo ulitanguliwa na maanadamano ya waendesha bodaboda, bajaji, magari ya kawaida na yale ya mafunzo ya udereva.
Polisi wa kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es Salaam, akiongoza maandamano ya magari wakati yakiwasili viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilayaya Temeke jijini Dar es Salaam, Bw. Felix Lyaviva akisalimiana na makamandawa polisi, Uhamiaji, Magereza, Zimamoto, viongozi wa dini na wajumbe wa baraza lausalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam.
Bw. Lyaviva akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, SACP, Gilles Mroto
Mkuu wa Wilaya akisalimiana na mjumbe wa baraza la usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Aziz Varda
Mkuu wa Wilaya akisalimiana na mjumbe wa baraza la usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Iddi Azan
Mkuu wa Wilaya akisalimiana na mjumbe wa baraza la usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum.
Mkuu wa wilaya akisalimiana na Makuu wa Uhamiaji wilaya ya Temeke
Mkuu wa Wilaya akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP, Salum Hamduni
Mkuu wa wilaya akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kionondoni, ACP Theopista Malya.
Mkuu wa wilaya akisalimiana na Mkuu wa magereza.
Mkuu wa wilaya akisalimiana na Kamanda wa polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Temeke, (RTO), ASP, Solomon Mwangamilo.
Polisi wa Usalama barabarani wakiwasili kwa maandamano.
Brass Band ya polisi ikiongoza maandamano.
Wanafuzni wa sekondari
Kwaya ya shule ikiongozwa na afisa wa polisi, ikihamasisha umuhimu wa kuzingatia sheria zausalama barabarani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: