Thursday, December 22, 2016

AIRTEL, VETA KUWAFIKIA VIJANA WA VIJIJI VINAVYONUFAIAKA NA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA), KUPITIA MTANDAO WA SIMU VSOMO

Diwani wa Bungu, Mhe. Ramadhan Mpendu (kushoto) akihamasisha wakazi wa Bungu kujiunga na VSOMO inayowezesha kutoa mafunzo ya ufunzi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu za mikononi kwa kushirikiana na Airtel katika semina iliyofanyika katika ofisi ya kata ya Bungu katika wilaya ya Rufiji.
Mhandisi wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO, Christopher Mbwiga (kushoto) akiwaelekeza wanakijiji wa kata ya Bungu juu ya mradi wa kusambaza umeme vijijini na kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi na kusoma kozi ya umeme kutoka VETA kupitia application ya simu za mkononi VSOMO itayosaidia kupata mafunzo yatayopelekea kupata ajira kwenye mradi huo katika semina iliyofanyika ofisi ya kata ya Bungu wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Afisa Mwendelezaji biashara SIDO, Stephen Bondo (kulia) akielekeza juu ya fursa za kibiashara kwa wanakijiji wa kata ya Bungu wilayani Rufiji zitokanazo na mradi wa kusambaza umeme vijijini REA na kuhamasisha wananchi kusoma kozi mbalimbali kutoka VETA kupitia application ya VSOMO itayosaidia kupata ajira na kujiajiri, katika semina iliyofanyika ofisi ya kata ya Bungu wilayani Rufiji.
Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa, Mhandisi Lucius R. Luteganya (wapili kushoto) akielezea utaratibu wa mafunzo ya ufundistadi kwa vutendo kupitia mradi wa Airtel na VETA wa unaotoa mafunzo ya ufunzi stadi kwa njia ya simu za mikononi, ujulikanao kama VSOMO kwa wanakijiji wa kata ya Bungu katika semina iliyofanyika katika ofisi ya kata hiyo katika wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani.
Mratibu wa kozi fupi na ujasiriamali VETA kipawa, Gosbert Kakiziba (kulia) akijibu nswali kutoka kwa wanakijiji juu ya kozi zipatikanazo kwenye application ya VSOMO inayowezesha kutoa mafunzo ya ufunzi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu za mikononi kwa kushirikiana na Airtel katika semina iliyofanyika katika kata ya Bungu wilayani Rufiji.
Albert Sahoya, Balozi wa Airtel kupitia mradi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, akitoa elimu ya jinsi ya kupakua application na kujiunga na mafunzo hayo kwa wanakijiji wa kata ya Bungu wilayani Rufiji.
---
Mamlaka ya ufundi stadi Nchini VETA kupitia chuo chake cha VETA Kipawa kimeanza kutoa mafunzo ya ufundi wa Umeme, ufundi wa simu za Mkononi, ufundi wa kuchomelea vyuma (welding) n.k katika vijiji vitakavyo nufaika na mradi wa Umeme Vijijini (REA) kwa kutumia njia ya mafunzo kwa njia ya simu ya Mkononi (VSOMO), mfumo uliobuniwa kwa pamoja kati ya Airtel na VETA na kuzinduliwa June 7, 2016.

Hayo yamesemwa katika uzinduzi wa program ya VSOMO uliobeba kauli mbiu (FURSA INAKUFUATA ULIPO) uliofanyika viwanja vya ofisi ya kijijini za kata ya Bungu Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani na Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa Eng. Lucius Luteganya kwamba “mfumo huu wa mafunzo (VSOMO), wanafunzi watajifunza nadharia kwa njia ya simu ya mkononi (smartphone) kwa kupakua bure mfumo huu wa VSOMO kutoka kwenye google play store ambapo msomaji atafanya mitihani ya kupima ufahamu wa somo kwa kutumia simu hiyo ya mkononi na hatimae mafunzo kwa vitendo kwa walio faulu nadharia, mafundi wa chuo cha VETA watawafuata wakiwa na karakana inayotembea (Mobile workshop) ili kutoa mafunzo ya vitendo kwa wale waliofaulu nadharia tu.

Eng, Luteganya aliongeza kuwa “Katika makubaliano yaliyofikiwa na wadau wengine, EWURA watatoa leseni kwa mafundi wa umeme watakaohitimu katika kozi ya UMEME, SIDO watatoa mafunzo ya ujasiliamali yanayoambatana na fursa za umeme kwa wanavijiji husika, na mwisho orodha ya wahitimu itapelekwa REA, TANESCO na kwenye Board ya wakandarasi ili mashirika na makampuni yatakayopewa kandarasi yaweze kuwatumia katika kujenga miundo mbinu (Wakandarasi), kutunza miundo mbinu (Tanesco) na REA”.

Katika uzinduzi wa Program hii (FURSA INAKUFUATA ULIPO) kwa wakazi wa vijiji vya Kata ya Bungu wilaya Rufiji Mkoani Pwani wadau wote VETA wakiwakilishwa na Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa Eng. Lucius Luteganya na timu yake, Airtel wakiwakilishwa na Bi. Hawa Bayumi Manager wa Airtel Fursa, SIDO wakiwakilishwa na Mr. Stephen Bondo, EWURA wakiwakilishwa na Chief Inspector Eng. Simon , Tanesco wakiwakilishwa na Eng. Mbwiga Chimala walipata mapokezi makubwa kutoka kwa wananchi na viongozi wa kata ya Bungu.

Nao baadhi ya Wananchi wameeleza kufurahishwa na mpango huo na kwamba mara nyingi wamekuwa wakishindwa kupata mafunzo kutokana na vyuo vya ufundi kuwa mbali lakini kwa sasa wanaona fursa hii imewafuata hivyo ni jambo muhimu katika maisha yao."Kusema ukweli haya mambo kwetu ni muhimu sana na mara nyingi tumekuwa tukishindwa kupata mafunzo kama haya kutokana na upatikanaji wake kuwa mgumu maana vyuo hadi usafiri kwenda Dar es salaam jambo ambalo ni gumu kwetu," Khamis Shaban-Mkazi wa Bungu

Nae Ramadhani Mpendu Diwani wa Kata ya Bungu ameeleza kufurahishwa na mpango huo huku akiwasisitiza viongozi wenzake kutoa elimu kwa wananchi ili wachangamkie fursa.hiyo muhimu na kuondoa malalamiko ya kuporwa ajira. Mfumo huu wa mafunzo utaendelea katika vijiji vingine vitakavyonufaika na mradi huu.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu