Friday, December 2, 2016

AIRTEL YAUNGANA NA SERIKALI KUTEKELEZA KAMPENI YA 'MTI WANGU'

Afisa Mazingira wa Manispaa ya Kinondoni, Awadh Jambo (kushoto) na Afisa Mazingira wa Airtel, Ncheye Mazoya wakipanda mti, wakati wafanyakazi wa Airtel waliposhiriki kupanda majani, miti na kuweka mbolea katika bustani iliyopo katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama “mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda.
Afisa Mazingira wa Airtel, Ncheye Mazoya akimwagilia mti baada ya kuupanda, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo, waliposhiriki kupanda majani, miti na kuweka mbolea katika bustani iliyopo katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama “mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda. Kushoto ni Afisa Mazingira wa Manispaa ya Kinondoni, Awadh Jambo.
Wafanyakazi wa Airtel wakishiriki kupanda miti katika bustani iliyopo katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama “mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda.
Baadhi ya wafanyakazi kwa pamoja wakipanda majani kwenye eneo la barabara ya Ali Hassan Mwinyi
---
Ongezeko la shughuli za kibindamu na viwanda kwa ujumla imesababisha kuongezeka kwa hewa ya ukaa na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi mfano mafuriko na joto kali ambalo husababisha magonjwa na athari kwa viumbe hai na binadamu kwa ujumla hasa katika miji mikubwa ikiwemo jiji la Dar es salaam.

Katika kutekeleza na kuunga mkono kampeni ya utunzaji wa mazingira maarufu kama “mti wangu” iliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es saalam , Mh Paul Makonda, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na wafanyakazi wake leo imeshiriki katika kupanda majani , miti na kuweka mbolea ili kutunza mazingira na kuyaweka katika hali ya kuvutia.

Bustani hiyo inayoanzia katika mataa ya Moroco hadi maeneo ya mgahawa wa Best Bite katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi ilikabidhiwa kwa kampuni ya Airtel na mh. Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kuboresha na kutunza mazingira ya jiji la Dar es saalam.

Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni hii, leo wafanyakazi wa Airtel kwa kushirikiana na serikali tunashirikia katika zoezi la kupanda majani na miti katika eneo la katikati ya barabara. Airtel tunaamini ili tuweze kufanya biashara tunahitaji mazingira bora na kwa kupitia kampeni hii ya mti wangu tunaunga mkono juhudi hizo kwa kuyatunza mazingira yanayotuzunguka na kuyaweka katika hali ya usafi na kuvutia” alisema Airtel Afisa Mazinga wa Airtel, Bwana Ncheye Mazoya

Kwa upande wake Afisa Mazingira wa wilaya ya Kinondoni, Bwn Awadhi Kinajambo alisema “tunatoa shukurani kwa kampuni ya Airtel kwa kuunga mkono jitihada hizi za kutunza mazingira kupitia kampeni hii mahususi ya “Mti Wangu”. Tunaanmini juhudi hizi zitasaidia katika kuboresha hali hewa,kuondoa tishio la majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kupendezsha jiji letu la Dar es salaam”.

Natoa wito kwa wakazi na wafanyabiashara wa maeneo haya kutokatiza kwenye bustani hii wala kutupa taka ili tuweze kuunga mkono kwa vitengo zoezi hili kuwa la mafanikio na kwa pamoja kutunza mazingara yetu.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu