Sunday, December 11, 2016

ALI KIBA, LADY JAYDEE NA DJ BONNY LOVE WANG'ARA TUZO ZA EATV 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikabidhi Tuzo ya Heshima kwa DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love baada ya kutangazwa mshindi wa heshima katika tuzo za EATV AWARDS 2016 zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love alipokuwa akitoa shukurani zake mara baada ya kupokea tuzo yake ya heshima iliyotolewa na EATV.

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Lady Jay Dee akipongezwa na Mpenzi mara baada ya kupokea tuzo yake katika hafla ya utoaji wa tuzo za EATV AWARDS zilizofanyika kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki Ali Kiba akipokea tuzo yake ya ushindiwa Wimbo Bora wa Mwaka kutoka kwa Nandi Mwiyombela kutoka kampuni ya Vodaco Tanzania katika Tuzo za Muziki za EATV AWARDS zinazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Lady Jay Dee akitumbuiza katika tuzo hizo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa EATV, Bi. Regina Mengi ambao ndyo waandaaji wa  tuzo hizo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu