Balozi Mteule, Dkt. Emmanuel John Nchimbi ametoa shukrani kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua nafasi ya kuwa balozi.

Kwa mujibu wa ukurasa wake wa mtandao wa Jamii, ameandika haya yafuatayo;

"Kwa Saa 48 nimetafakari imani kubwa aliyoionyesha kwangu mhe Rais John Pombe Magufuli kwa kuniteua kuwa Miongoni mwa mabalozi wetu, nimetafuta maneno muafaka ya kumshukuru na kumuonyesha ninavyoithamini imani yake kwangu lakini nimeyakosa.

Mhe Rais naomba upokee neno langu moja tu "ASANTE"
Nitafanya kazi kwa juhudi na maarifa kufikia matarajio yako kwangu.

Kwa watanzania wenzangu nimepata maelfu ya salaam za kunipongeza na kuniombea kheri nawashukuru Sana, sitawaangusha.

Mwisho Namshukuru Kipekee Mwenyezi Mungu kwa kufanya niendelee kuaminiwa naomba aendelee kunisaidia niilinde imani niliyoonyeshwa".
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: