Thursday, December 22, 2016

BARAKA DE PRINCE, MC PILIPILI NA ROSE NDAUKA KUPAMBA TAMASHA LA CHRISMASS KIDS, DODOMA

 MSANII wa kizazi kipya Baraka Da Price pamoja na Mwigizaji maarufu wa Bongo Movie, Rose Ndauka wamesema kuwa wamejiandaa vema kumsindikiza Mchekeshaji maarufu nchini, Emanuel Matebe a.k.a Mc Pilipili katika Tamasha la Chrismass la kids Festival litakalofanyika mkoani Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square Desemba 25 na 26 mwaka huu.

Wasanii hao pia Desemba 26 mwaka huu watatoa burudani nyingine kama hiyo katika ukumbi wa royal village na kuwapa fursa watu wa Dodoma kupiga picha na Tuzo aliyoipata McPilipili ya Mshereheshaji bora wa mwaka 2016.

Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari, Muigizaji nguli Rose Ndauka alisema kuwa tamasha hilo litakuwa la kipekee katika mkoa wa Dodoma ambapo ataweza kupanda jukwaani pamoja na Mchekeshaji huyooo na kutoa burudani ya aina yake.
 Alisema pia ataamua kuongea ukweli juu ya uhusiano wake na Mc Pilipili katika tamasha hilo kwani watu wengi wamekuwa wakiandika katika mitandao mbalimbali ya kijamii juu ya ukaribu waliokuwa nao.

"Nataka kuwaambia watu wangu wa Idodoma kule kwa kina Mc.Pilipili mkae tayari kwa ujio wangu kwani siku hiyo ndio itakuwa siku yangu maalum ya kupanda jukwaani na Mc.Pilipili katika kuhakikisha nina wavunja mbavu, Mashabiki zangu naombeni mjitokeze kwa wingi kuitikisa siku hiyo Dodoma na viunga vyake,"alisema

Kwa Upande wake Emanuel Matebe a.k.a Mc Pilipili alisema tamasha hilo litakuwa ni tamasha la aina yake kwani litawakutanisha wasanii mbalimbali nchini wa muziki wa kizazi kipya pamoja na waigizaji wakiwemo Baraka da Price, Rose Ndauka ,Katarina Karatu pamoja na Casto.

Alisema katika tamasha hilo Decemba 25 mwaka huu watoto wataweza kuingia kwa kiingilio cha shilingi 2000 huku wakubwa sh.5000 huku katika tamasha la Desemba 26,kutakuwa na kiingilio cha VIP ikiwa 30000 na kawaida 10000.

"Nawakaribisha ndugu zangu wa Dodoma katika matukio haya mawili siku hiyo itakuwa siku ya pekee kwangu kuonyesha kipaji changu nyumbani hivyo nitahakikisha nawatendea haki ipasavyo huku nikirudisha tuzo ya Mshereheshaji bora nyumbani niliyopewa katika tuzo za Insta Award ambayo mashabiki zangu watapata fursa ya kupiga nayo picha," alisema.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu