Utasikia watu, eti, watumie watu 10 utaingia peponi. Au mambo yako yatakuwa mazuri, hivi mnadhani Pepo mchezo!

Yohana mbatizaj aliishi hadi mapangon kwa kula asali na nzige kwa ajili ya kuitangaza injil,

Mtakatifu Yohana yule mwanafunzi wa Yesu, alikaangwa kwenye mafuta yanayochemka, baadae akatupwa kwenye kisiwa cha mateso cha patmo mpaka akafunuliwa mambo mazito na magumu

Isaya aliuwawa kifo cha kukatwa vipandevipande kwa msumeno wa kukatia mbao akiwa hai.

Stephano alipigwa kwa mawe mpaka akafa

Daniel alitumbukizwa kwenye tundu la simba sababu ya kuishindania imani, Yusuph ilimbidi kwenda gerezani kwa sababu ya kuulinda utakatifu wake, Shedrack, Meshack na abelnego walitumbukizwa kwenye tanuru liwakalo moto. Yote hii ni kwa sababu ya kuisimamia imani

Leo hii anatokea, mtu, kwa meseji yake isiyo na mashiko wala vina alafu anakutisha, anakulazimisha utume kwa watu 10 maisha yako yatakuwa mazuri, au eti mm ni Yesu/Mtume Mohammad S.A.W nakuagiza tuma ndani ya dk 3.

Unadhani mbinguni ni kariakoo? kwa sms yako tu ukale bata mbingun, halafu unategemea uingie Peponi, tusidanganyane, Pepo sio mas'hara ndugu yangu, sio maneno matupu na sms nyingi.

Tumche Mungu kisawasawa.

WAKUMBUSHE WANAOGAWA PEPO KWA SMS..
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: