Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick moja ya kompyuta sita zilizotolewa na taasisi yao kwa mkoa huo kama msaada wa kuweza kuongeza utendaji kazi mzuri kwa watumishi wa umma, hususan kwa Manispaa ya Moshi, Halmashauri ya Mwanga na Halmashauri ya Same, huku kila moja ikipewa kompyuta mbili. Kushoto kwa RC Sadick ni Katibu Tawala wa Mkoa huo wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Aisha Amour. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

HALMASHAURI ya Wilaya Same imeanza kupokea faraja za msaada wa kompyuta mbili kati ya sita zilizofikishwa mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi yao kuungua moto na kutekeza vifaa mbalimbali vya kiofisi.

Kompyuta hizo zilipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick, akiambatana na wakuu wa idara wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watumishi mbalimbali kutoka kwenye halmashauri za Same na Mwanga.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick wa pili kutoka kushoto, akimkabidhi kompyuta hizo alizopokea kwa Taasisi ya Bayport Financial Services, Katibu Tawala wake wa Mkoa, Mheshimiwa Aisha Amour.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika hafla ya kupokea kompyuta hizo, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema wamekabidhi kompyuta hizo, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Same kuungua moto.

Alisema ingawa msaada wao umekuja kabla ya ofisi hizo kuungua moto, lakini wanaamini kuwa kompyuta hizo zinaweza kupunguza adha ya watumishi wa umma kufanya kazi kwa wakati mgumu, huku zikilengwa kwa Halmashauri ya Same, Mwanga na Manispaa ya Moshi.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Said Mecky Sadick katikati akizungumza jambo na Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa kulia bada ya kukabidhiana kompyuta sita za msaada kwa Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Said Mecky Sadick kushoto akimkabidhi kompyuta mwakilishi wa Halmashauri ya Same.

“Taasisi yetu inatoa pole kubwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na watumishi wote wa Same, ila tunaamini kwa kiasi kidogo kompyuta tulizotoa zitawafuta machozi wadau wenzetu wa Same na Serikali yote kwa ujumla hapa nchini,” alisema Mercy.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Mecky Sadick, aliwashukuru sana Bayport kwa msaada wao wa kompyuta na kuwataka waendelee kuwasaidia watumishi wa Same kwa kuongeza idadi ya kompyuta zao.

“Tunapokea kompyuta hizi kwa mikono miwili lakini tunawaomba wenztu wa Bayport muongeze idadi ya kompyuta kwa Halmashauri ya Same kwa sababu kule kuna uhitaji mkubwa zaidi baada ya ofisi kuungua moto.

“Ofisi yetu imepata pigo kubwa mno hivyo mtusaidie kwa hilo kwa sababu tunafahamu msaada wenu ni muhimu kwetu na taasisi yenu imekuwa karibu sana na jamii kwa kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii ambayo yana tija kwetu sote,” alisema RC Sadick.

Utaratibu wa utoaji wa kompyuta 205 kwa ofisi za serikali zenye thamani ya Sh Milioni 500 umeanzishwa ili kuwafanya watumishi wa serikali wafanye kazi zao kwa ufanisi ili kuhamasisha masuala ya kimaendeleo hapa nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: