Thursday, December 22, 2016

JESHI LA POLISI LAIMARISHA ULINZI KUELEKEA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA 2016


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Jeshi la polisi limesema limeimarisha ulinzi kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Akizungunza leo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema Jeshi la Polisi katika kipindi za sikukuu kuna watu wanajipanga kufanya uhalifu hivyo jeshi litafanya doria za kutosha.

Amesema kumbi zote zinazofanya starehe za kupiga mziki ziingize watu kutokana na ukumbi na watakaozidisha watachukuliwa hatua.

Afande Advera amesema wataoendesha vyombo vya moto huku wamelewa wakibainika watachukuliwa hatua kutokana kufanya hivyo nikutaka kusababisha ajali.

Aidha amesema wazazi wanatakiwa kufanya ulinzi kwa watoto kutokana kuwepo na watoto wengi katika vituo vya polisi wakiwa wamepotea.

Hata hivyo amesema wananchi watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapohisi kuna watu wanaoashiria kufanya uhalifu.

Advera amesema kuwa wale ambao watatoa taarifa zikashindwa kutekelezeka wawasiliane na ngazi ya juu ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa watu waliofanya uzembe.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu