Thursday, December 1, 2016

KAMPUNI MAARUFU YA FILAMU YA UJERUMANI KUPAISHA SEKTA YA UTALII NCHINI

Moja ya eneo la lililotumiwa na kampuni ya Polyphon Film ya nchini Ujerumani ikirekodi Filamu inayozungumzia maisha kwa ujumla eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti mkoa wa Mara na inatarajiwa kukuza utalii.
Eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo picha za video za sehemu ya Tamthiliya ya Dream Boat zimepigwa hapo.
Moja ya gari lililotumika katika tukio hilo likitoka eneoo la tukio kando ya Mto Mara unopita katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Uchukuaji wa picha za video kando ya Mto Mara ukiendelea.
Mkurugenzi wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini Arusha (kushoto), Gabriel na Meneja Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film, Manuel Shrouder wakiwa eneo la kutengeneza filamu hiyo itakayooneshwa kwenye kituo maarufu cha Runinga cha ZDF nchini Ujerumani na kutazamwa na zaidi ya watu 10 milioni katika nchi tatu zikiwemo Austria na Uswizi.
Meneja Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Manuel Shrouderk (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa)Ndg Ibrahim Mussa(katikati) anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini Arusha, Gabriel.
Mratibu wa Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film, Mona Lessink akizungumza na waandishi wa habari kuhusu filamu hiyo itayoanza kurushwa katika kipindi cha Pasaka mwaka 2017, kushoto ni Meneja Uhusiano wa Tanapa, Pascal shulutete akifatilia kwa karibu.
Sehemu ya magari yaliyobeba vifaa vya kutengeneza filamu hiyo ambayo imegharimu kiasi cha Euro 1.7 milioni.
Wataalamu wa kampuni hiyo wakiwa eneo la kutengeneza filamu ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Askari wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa Serengeti wakiimarisha ulinzi kwa wageni hao.
Katika kuboresha filamu hiyo upigaji wa picha kwa kutumia ndege ndogo ili kuonyesha madhari ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ulifanyika chini ya usimamizi wa Tanapa.
Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa (katikati) akizungumza na Mratibu wa uzalishaji wa filamu wa kampuni ya Polyphon ya nchini Ujerumani, Mona Lessnick alipotembelea eneo la Kogatende jirani na Mto Mara ambapo kulikuwa kukifanyika shughuli za uchukuaji wa picha za video kwa ajili ya Tamthiliya ya Dream Boat. kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA, Pascal Shelutete.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiteta jambo na Mona Lessnick katika eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkurugenzi wa Utalii wa TANAPA, Ibrahim Musa( katikati) akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Jorg Gabriel walipoktana eneo la Kogatende katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete akisaidia kubeba moja ya Kamera kubwa zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uchukuaji wa picha katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Moja ya Kamera kubwa iliyokuwa ikichukua matukio katika upigaji picha wa Tamthiliya ya Dream Boat katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkurugenzi wa Utalii akiitizama Kamera ambayo ilikuwa iktumika kupiga picha za matukio mbalimbali wakati wa utengenezaji wa filamu hiyo.
Wataamu wakifunga Kamera katika ndge ndogo ya Shirika la ndege la Costal Airline kwa ajili ya upigaji wa picha za juu. Picha zote na Dixon Busagaga na Emmanuel Filbert.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu