Tuesday, December 20, 2016

MAKATIBU WAKUU WAKABIDHIANA OFISI JIJINI DAR


Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akimkabidhi nyaraka za uendeshaji na usimamizi wa utumishi wa umma Dkt. Eng. Maria Sasabo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Makabidhiano yamefanyika Ofisini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na kushuhudiwa na watumishi wa Wizara hiyo.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akimkabidhi ofisi Dkt. Eng. Maria Sasabo, Katibu Mkuu wa Mawasiiano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Prof. Faustin Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano ambapo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemhamishia Ofisi ya Makamu wa Rais. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Eng. Maria Sasabo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Aidha, Eng. Anjelina Madete amewasili rasmi Wizarani hapo na kushuhudia makabidhiano hayo baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano. Awali Eng. Anjelina Madete alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Makabidhiano yamefanyika Ofisini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na kushuhudiwa na watumishi wa Wizara hiyo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu