Thursday, December 29, 2016

MBUNGE MWAMOTO ACHANGIA MILIONI 20 MIRADI YA MAENDELEO KILOLO

Mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto wa tatu kulia akiongozana na kamati yake ya mfuko wa jimbo kukagua miradi ya kimaendeleo na kuchangia miradi hiyo pichani ni jengo la maabara ambalo limekwama kuendelea katika shule ya Sekodari Ipeta
Mbunge Mwamoto akitazama shughuli za ujenzi wa vyoo katika shule ya Msingi Iramba
Mbunge wa kilolo Venance Mwamoto akikagua ujenzi wa choo cha wanafunzi shule ya Msingi Iramba jana wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbali mbali jimboni humo
Mwamoto akikagua ujenzi wa kituo cha Afya Ukumbi.
Shimo la choo shule ya Sekondari Ipeta.
Vyumba vya madarasa shule ya msingi Italula.
Vyoo vya zamani vya wanafunzi shule ya Msingi Kidabaga.
Ujenzi wa vyoo vya kisasa shule ya Msingi Kidabaga ukiendelea.
Majengo ya shule ya Msingi Kidabaga.
Maabara ya shule ya sekondari Ipeta ikiwa imesimama ujenzi wake.
Choo cha mwalimu mkuu shule ya Msingi Mdeke Kilolo

Na MatukiodaimaBlog

MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Venance Mwamoto amechangia zaidi ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha miradi mbali mbali ya kimaendeleo ikiwemo ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi, madarasa, nyumba za walimu na Zahanati.

HAyo ameyasema jana wakati alipofanya ziara ukaguzi wa miradi 9 inayoendelea kwa nguvu za wananchi na Halmashauri ya wilaya ya Kilolo na kueleza kuvutiwa na miradi hiyo japo kuna hitajika msukumo wa haraka katika umaliziaji wa miradi hiyo.

Mhe. Mwamoto aliwataka viongozi wa kijijini kusimamia ujenzi kwa uaminifu na akaongeza atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.

Alisema kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya kwa mvua kuchelewa kunyesha katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Kilolo tofauti na miaka mingine ameona ni vema kuwapunguzia makali ya michango wananchi wake na badala yake sehemu ya michango ambayo walipaswa kuchangia ili kukamilisha miradi hiyo kuibeba yeye kupitia mfuko wa jimbo.

"Ninawaombeni sana wananchi wangu kwa sasa ninyi mshiriki zaidi katika maendeleo kwa kuchangia nguvu zenu na mimi niwaunge mkono kwa kuchangia fedha ili kuifanya miradi hii ikamilike kwa wakati"

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu