Friday, December 16, 2016

MICHEZO YA TANO YA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA YATIMUA VUMBI ,TANGA

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deudence Kakoko, amewataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kwenda kasi ya Serikali ya awamu ya Tano.

Akifungua michezo ya Tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS GAMES) viwanja vya shule ya Sekondari ya Popatlal Tanga jana, Kakoko, alisema kila mfanyakazi wa Mamlaka hiyo anapaswa kujua wajibu wake.

Alisema kasi hiyo iende sambamba na uboreshaji wa utoaji huduma bandarini na kuwa kivutio kwa wageni ili kuweza kuitumia kwa kushusha shehena zao bandari za Tanzania.

Michezo hiyo inashirikisha wafanyakazi wachezaji kutoka Tanga ambao ni wenyeji, Dar es Salaam,, Mtwara na Bandari za Ziwa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu