Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimwapicha Mkuu wa Wilaya ya  Ubungo, Kisari Matiku Makori kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli  kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni. Leo jijini Dar es Salaam. Picha na  Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisari Matiku Makori akila kiapo mbele ya Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais  Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkabidhi katiba na ilani ya  chama cha mapinguzi (CCM) Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisari Matiku Makori  mara baada ya kumwapisha leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya wa mkoa wa Dar es Salaam, leo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na
kamati ya ulinzi na usalama ya jiji la Dar es Salaam.
---
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemuapisha Kisari Matiku Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni.

Akimuapisha Mkuu huyo wa Wilaya RC Makonda ameeleza kuwa wananchi wa Ubungo wanamatumaini na uteuzi wake na lengo kuu la kuanzisha wilaya ya Ubungo ni kusogeza huduma za wananchi karibu hivyo inabidi ahakikishe anatatua changamoto zao kwa kuwafuata huko waliko na asiridhike na ripoti anazoletewa ofisini kwani kumekuwepo na changamoto kubwa ya uwajibikaji hivyo inabidi hajiridhishe kwanza.

Katika hatua nyingine RC Makonda amewaagiza wakuu wa wilaya wote kutoruhusu wananchi kubomolewa nyumba zao mpaka kuwepo hukumu halali ya mahakama kwani wananchi wamekuwa wanaonewa na kudhulumiwa haki zao, hivyo wakuu
wa wilaya kwa kushirikiana na jeshi la polisi wahakikishe haki inatendeka kwa kufuatilia ukweli na kujiridhisha kwa kuzikagua nyaraka husika.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya huyo Makori ameomba ushirikiano kwa viongozi wenzake ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu na kuahidi kuwa atafanya siasa za kuleta maendeleo ili kila mwananchi anufaike na rasilimali zilizopo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: