Saturday, December 31, 2016

MNYIKA APINGA ONGEZEKO LA BEI YA UMEME 8.5%

 
Napinga ongezeko la bei ya umeme 8.5% lililotangazwa na EWURA kwa kuwa ni mzigo kwa wananchi na uchumi wa nchi na sababu zilizotolewa hazina msingi.

Namtaka Waziri Muhongo atengue uamuzi huo mbovu kama alivyoahidi kwamba hatarusu bei ya umeme kupanda.

Natoa mwito kwa Rais Magufuli naye katika hotuba yake kwa taifa leo au kesho azungumzie ongezeko hilo.

Iwapo Waziri au Rais hawatatoa kauli nitalifikisha suala hilo bungeni kwa hatua zaidi.

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu