Saturday, December 17, 2016

MPOGOLO AKAGUA MALI ZA CCM MKOANI DODOMA

Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo (Kulia), kuhusu jengo la ukumbi wa mikutano la CCM, lililopo Kilimani mjini Dodoma, Mpogolo alipotembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kukagua mali za CCM, leo Desemba 17, 2016. Kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki.
Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, akimuonyesha mwisho wa shamba la CCM, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (wapili kulia), Mpogolo alipokagua kiwanja hicho kilichopo eneo la Kilimani mjini Dodoma, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, leo Desemba 17, 2016, mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, wakati wakiizunguka kuikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo Desemba 17, 2016.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimhoji jambo Fundi wa magari ya Chama, Ramadhani Mbelwa (kushoto), alipokuwa akikagua magari mabovu ya Chama, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo Desemba 17, 2016. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi. (Picha na Bashir Nkoromo)

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu