Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (kulia), akitoa taarifa fupi ya mradi huo mbele ya mgeni rasmi.
Meneja Huduma kwa Wateja wa MSD, Salome Malamia akizungumza katika hafla hiyo.
Mmoja wa maofisa kutoka Ofisi ya Inayosimamia Utekelezaji wa Mapendekezo ya Maboresho (SMO), Naomi Shangali akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu mpango huo.
Ofisa wa SMO, Frankie Nkone akieleza kazi za eneo lake zinavyofanyika.
Wajumbe wa mkutano huo kutoka sekta ya afya wakiwa wameinamisha vichwa vyao kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, marehemu Profesa Idris Mtulia aliyefariki jana.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa SMO.

Na Dotto Mwaibale.

BOHARI ya dawa (MSD) imezindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wake wakubwa, kama moja ya hatua za kuboresha huduma kwa wateja.

Mpango huo utawawezesha wateja hao kupata huduma ya haraka zaidi pindi wanapokuwa wanahitaji mahitaji yao.

Wateja hao ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Hosipitali ya Sekoutoure Mwanza, Hospitali ya Kibong’oto, Mirembe, Hosipitali za Amana, Temeke, Mwananyamala, KCMC, Hospitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Akizindua mpango huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya amesema mpango huo ni moja ya maboresho yanayofanywa na MSD, ili kuhakikisha huduma zake zinatolewa kama inavyohitajika.

Dk. Mpoki pia amewasisitiza wateja hao wakubwa wa MSD kuhakikisha wanafanya maoteo sahihi ya mahitaji yao na kuyaleta MSD kwa wakati ili kuepusha ucheleweshwaji wa taratibu za manunuzi ambao pia itasababisha dosari kwenye upatikanaji wa dawa kwa wateja.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu amesema hatua ya kuwahudumia wateja hao kwa kiwango kizuri na cha uhakika itafanikiwa, hivyo Watarajie maboresho makubwa ya huduma ya upatikanaji wa dawa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: