Monday, December 26, 2016

MWANAFUNZI ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHALANGWA MAPANGA NA MWALIMU

Marco Limbe akiwa amepoteza fahamu huku akipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Nyashimo.

Na Shushu Joel, BUSEGA - SIMIYU.

MWANAFUNZI Marco Limbe (14) aliyemaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya msingi Yitwimila iliyoko kata ya Kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu amelazwa katika kituo cha afya Busega mara baada ya kuchalangwa mapanga kichwani na mdomoni na mwalimu wake.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akirejea nyumbani kwao akitokea katika malisho ya mifugo ndipo alipokaribia katika shamba la mwalimu Pendo Gabriel ndipo mwalimu huyo alimkamata kijana huyo na kuanza kumchalanga kwa panga na kupelekea kijana limbe kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 mara baada ya kufikishwa katika kituo cha afya Busega.

“Shuhuda wa tulio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Manoga anaeleza kuwa ilikuwa kama mchezo lakini kumbe ni kweli kwani niliona mifugo ya limbe iliyokuwa ikielekea nyumbani na huku limbe akiwa nyuma ya mifugo hiyo katika barabara ambalo liko karibu na maeneo ya shule ghafla nilimuona mwalimu pendo wakishikana na kijana huyo na ndipo nikamuona akiwa na panga na kuanza kumchalanga”
Mwalimu pendo akiwa amelazwa mara baada ya kupokea kichapo toka kwa wananchi mara baada ya kumchalanga mwanafunzi wake kwa panga.

Nilikimbia katika tukio na kutoa msaada kwa wote lakini mara watu walijaa na kuanza kumshambua mwalimu Pendo kwa kumpiga ingawa jaribio hilo lilikwama mara baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho mshemas bahai.

Nipashe ilikwenda katika kituo cha afya cha Nyashimo na kujionea hali mbaya kwa kijana Limbe ambaye alikuwa amepoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 bila kujitambua na huku akiwa anaongezewa drip na kwa pembeni mwalimu Gabriel naye akipata matibabu ya jeraha lake kichwani amabolo alishambuliwa na wananchi na huku akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la piolisi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio mwenyekiti wa Sogesca Bahai Mshemas alisema kuwa sikukuu ya kuzaliwa kwa yesu imekuwa ni mbaya katika kijiji chake mara baada ya wananchi walio na hasira kali kufanya shambulio la kumshambulia mwalimu Pendo kwa kosa la kumchalanga na panga mwanafunzi wake aliyekuwa akitokea kwenye malisho na kupita karibu na shamba lake la mahindi.

Aliongeza kuwa alifanikiwa kuwatuliza wananchi wa kijiji chake na kuanza kufanya mikakati ya kuwapeleka kituo cha afya ili wapate huduma za matibabu.

Aidha Mshemasi aliongeza kuwa walifika polisi na kuandikiwa barua ya kwenda kutibiwa wote wawili mwalimu pamoja na mwanafunzi.

Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho cha afya Dk. Ayubu Ismail alithibitisha kuwapokea kwa majeruhi hao na kudai kuwa kijana limbe ndiye aliyekuwa na hali mbaya zaidi kuliko mwalimu pendo.

Aliongeza kuwa kijana ameshonwa nyuzi 9 katika sehemu zake zote alizopatwa na majeraha na huku mwalimu yeye akiwa ameshonwa nyuzi 6.

“ni kweli Limbe alikuwa ametokwa na damu nyingi sana na hivyo kumpelekea kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 lakini hali yake inaendelea vizuri alisema Dk Ismail”

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu