Mbali ya kuwa Sikukuu ya Krismasi kwa Wakristo duniani, pia jana Disemba 25,2016 ilikuwa siku ya furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Bwana harusi Mathew Akrama Rwekila na Bibi harusi Agnes Martine (wawili katikati), baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.

Bibi harusi ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Jijini Mwanza, akifahamika zaidi kwa jina la Agnes Akrama, wote wakimtumikia Mungu katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.

Picha na Craty Cleophace.
Maharusi na wasaidizi wao, wakimsikiliza Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpywa, Dkt.Daniel Moses Kulola, wakati wa ibada yao
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akisisitiza jambo wakati wa ibada ya ndoa.
Bwana harusi Mathew Akrama Rwekila na Bibi harusi Agnes Martine, wakila kiapo cha ndoa.

"Mungu akasema, Si vyema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye". Mwanzo 02:18. Tazama picha zaidi HAPA
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: