Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi (katikati), akizungumza kwenye mkutano huo.
Blogger kutoka mkoani Arusha, Tumaniel Seria (kulia) akitoa shukrani mara baada ya mgeni rasmi kusema neno.
Picha ya pamoja.
---
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

SERIKALI imesema itachukulia sheria vyombo vyote vya habari ambavyo vitatumia picha ama habari kutoka blog yoyote ile bila ya adhini ya mmiliki ama kutaja wapi amepata habari hiyo.

Kauli hiyo imetolewa namkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Hassan Abbasi, alipokuwa akijibu hoja za wamailiki wa mitandao ya globu nchini ambao wamekutana kwa mkutano wa siku mbili katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam.

“Magazeti ama chombo chochote cha habari ambacho kitachukua picha ama habari kutoka kwenye blog yoyote bila ya ruhusa ya mwenye ama kumtaja kama sheria inavyotaka basi achua za kinidhamu zitachukuliwa kama inavyohitajika na matakwa ya sheria” Amesema Abbas.

Abbasi ametoa rai kwa wamiliki wa vyombo vya habari kuwa kama watafanya kinyume na hivyo sheria itafata mkondo wake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: