Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango (kulia), akikata utepe kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuashiria kuzindua rasmi Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa GEPF, Joyce Shaidi.
Mwonekano wa ukumbi wa mikutano wa kituo hicho.
Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, akisalimiana na wageni waalikwa.
Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango (wa tatu kushoto), akiwa na viongozi wengine akitoka kukagua vyumba vya kupumzikia vya kituo hicho.
Wanataalumu ya Uhasibu wakiwa kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa kituo hicho pamoja na kongamano lao la 2016 la siku tatu.
Wasanii Mpoto Mrisho na Banana Zoro wakitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo, akitoa taarifa fupi.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi.
Picha ya pamoja.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imeitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kutoa hadharani majina ya wahasibu wabadhilifu ili jamii iweze kuwatambua.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Dk.Philip Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizindua Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju na Kongamano la Uhasibu la 2016 la siku tatu Dar es Salaam leo.

"Ni vizuri mkaanza kutoa hadharani majina ya wahasibu wasio waadilifu ili jamii iweze kuwajua" alisema Mpango.

Mpango alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutaisaidia serikali kuelekeza fedha zilizokuwa zikitumika na bodi hiyo kukodi kumbi kwa kazi zake mbalimbali kupelekwa kufanya kazi zingine za maendeleo.

"Nawaombeni mkitunze kituo hiki ili kitimize malengo yake ya kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla" alisema Mpango.

Aliwataka wahasibu nchini kutumia taaluma yao kuisaidia serikali hasa katika kipindi hiki cha nchi kuelekea kwenye uchumi wa viwanda badala ya wao kushirikiana na wafanyabishara wasio waaminifu kuiibia serikali.

Mpango alisema kuwa serikali itaendelea kuwatumbua watumishi wasio waaminifu na wahasibu bila ya kumuonea muhusika huruma na kuwa atakayebainika atapelekwa mahakama ya mafisadi iliyofunguliwa.

Mkurugenzi Mkuu wa NBAA Pius Maneno alisema katika kipindi cha maiaka 12 iliyopita walikuwa wakitumia sh. biliobi 1.5 kwa ajili ya gharama za kulipia kumbi hivyo ujenzi wa kituo hicho utaondoa changamoto hiyo na kuwa kitakuwa ni chanzo cha mapato.

Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Profesa Isaya Jairo alisema kituo hicho kimejengwa kwa mkopo wa sh.bilioni 15 kutoka Shirika la Hifadhi ya Taifa (NSSF), Mfuko wa GEPF bilioni 10 na Wahasibu na Wakaguzi walichangia Bilioni 8.

Alisema awali walikadiria ujenzi huo ungekamilika kwa gharama za sh. bilioni 14 lakini kutokana na sababu mbalimbali kukamilika kwake kumefikia sh. bilioni 33 zaidi ya kiasi kilichokuwa kimepangwa.

Mwenyekiti wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi aliishukuru serikali kwa ushirikiano na mifuko ya jamii na NBAA hasa katika suala zima la kusukuma maendeleo ya nchi ikiwa na kuzitaka taasisi zake kwenda kukodi ukumbi wa kituo hicho cha kimataifa ili kusaidia kurejesha fedha zilizokopwa kukijengea.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: