Tuesday, December 13, 2016

SIJAUACHA MUZIKI, UMAMA LISHE NAO UNALIPA - SHILOLE

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, amegeukia kazi ya mama lishe na kuanza kuuza chakula, kwa staili ya kuwapelekea wateja wake walipo.

Shilole alisema biashara hiyo anaamini itakuwa na wateja wengi na itamwingizia kipato tofauti na mastaa wengine ambao wamekuwa waking’ang’ania biashara zisizokuwa na tija ilimradi waonekane tu.

“Mimi nafanya biashara ambayo nina uhakika nayo ya kupata wateja na baada ya muda nitajua faida ninayoipata, mimi napambana kujenga maisha yangu,” alisema mkali huyo wa miondoko mbalimbali ya muziki na mcheza filamu maarufu.

Msanii huyo licha ya umaarufu mkubwa lakini amekuwa akijichanganya kushiriki masuala mbalimbali ya kibiashara huku mwenyewe akidai kwamba staili hiyo ndiyo itakayomfanya anufaike na ustaa wake badala ya kukaa ndani na kuwa tegemezi.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu