Saturday, December 31, 2016

TUTUMIE GHARAMA KUBWA KATIKA KUSAIDIA MAENDELEO NA MAISHA YA WALIO HAI


Wabongo mtu akiwa anaumwa au kupata tatizo ambalo linahitaji hela, faraja au vyote ili awe sawa huwa tunaficha au kuuchubua au tunauchuna.

Ila akishakufa tu, utaona hata uliyekuwa unamdai nae atakupa hela zote na cha juu kwa ajili ya kufanikisha msiba na mazishi yako (HUU UPUMBAVU SIUKUBALI)

Mimi binafsi ukiwa unaumwa au una tatizo ambalo unahisi unahitaji msaada wangu niambie na nitajitahidi kukusaidia, Ila ukifa unaweza hata usipate jero yangu, maana ushakufa na huna faida na Mimi na hata Mimi nikiwa hai ninapohitaji msaada wako nisaidie sio mpaka nife ujidai eti ulikuwa karibu sana na Mimi na unanipenda wakati nilipokuwa hai nimeshakuomba sanaa msaada mara kibao ukauchubua au kunitosa japokuwa uliweza nisaidia nisife,

Maana hata nikifa kunizika kwenye jeneza la gharama na sherehe ya mazishi kutumia hela nyingi naona huo ni upumbavu wa hali ya juu, maana nikifa hata ukitupa mwili wangu popote pale hakuna binadamu au nzi au funza atakaevumilia harufu yangu hivyo naamini nitazukwa tu.

TUTUMIE GHARAMA KUBWA KATIKA KUSAIDIA MAENDELEO NA MAISHA YA WALIO HAI.

Raymond BillGates Maganga.
Heri ya mwaka mpya 2017
Amen.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu