Na Ripota wa Globu ya Jamii, Mbeya.

Wananchi wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wamevamia kituo cha Polisi Jeshi la Polisi cha makongolosi kwa kufanya fujo na uwarushia mawe polisi wa kituo hicho kwa lengo la kuwatoa watuhumiwa wa kituo hicho wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji.

Akizungumza baada ya tukio hilo , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Polisi Dhahiri Kidavashari, amesema kuwa mnamo desemba 18, mwaka huu Kundi la wananchi Mkoani Mbeyilaya ya Chunya, Tarafa ya Kiwanja, Kata ya makongolosi Wananchi waliamua kujichukulia sheria mkononi kwa kuvamia kituo cha Polisi Makongolosi na kufanya fujo kwa kuwarushia mawe askari wa Kituo hicho kwa lengo la kuwatoa watuhumiwa wawili waliokuwa katika kituo hicho.

"Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu ili kuhakikisha matukio ya namna hiyo kuisha kabisa."

Aidha amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Erasto Robert, [28] mkazi wa Kilombero na Basil Linus [24] mkazi wa Makongolosi wanaodaiwa kukabiliwa na kosa la mauaji kwa RB namba [MKI/IR/1249/2016] kwa lengo la kuwatoa nje na kuwauawa kwa kuwachoma moto.
Amesema kuwa inadaiwa wananchi hao walifika Kituoni hapo kwa lengo la kuwatoa nje watuhumiwa hao wawili lakini, Diwani wa Kata ya Makongolosi Bwana Lusajo Ntofyo aliweza kuongea na wananchi hao na kisha kutawanyika, Hata hivyo wananchi hao walifunga barabara ya Chunya-Makongolosi kwa kuweka mawe makubwa na magogo hali iliyosababisha usumbufu mkubwa wa watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Aidha katika vurugu hizo watu wanne walijeruhiwa ambao ni Dimita Mwangabula [24] fundi uashi, mkazi wa Makongolosi [aliumia miguuni na mikononi] 2. Amosi Kandonga [16] mkazi wa Kasumulu Wilaya ya Kyela [aliumia puani] 3. Hawa Masumbuko [21] mkazi wa Makongolisi [aliumia mkononi wa kulia] na 4. Amoke Mbilinyi [25] mkazi wa Makongolisi ambao walikimbizwa hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa matibabu.
Hata Hivyo mbali Matukio hayo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya pia linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatii sheria za usalama barabarani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi Dhahiri Kidavashari ametoa wito kwa wananchi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kwani vinasababisha madhara makubwa kwa watu wasiokuwa na hatia na usumbufu kwa wengine.
Sehemu ya Askari Polisi wa Mkoa wa Mbeya wakifanya ulinzi katika eneo la tukio.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: