Monday, January 2, 2017

BABA RAIS DKT. MAGUFULI 2016 UMETUPA RAHA WATANZANIA

1. Baba Magufuli kwa kweli nimeshindwa kuvumilia lazima nikwambie wewe ni balaa yani khaaa!! Ndani ya mwaka mmoja pamoja na mtikisiko wa uchumi duniani wewe umeongeza mapato ya mwezi kutoka Bilioni 900 hadi Trilioni 1.2;

2. Ndani ya mwaka mmoja watalii waliokuwa hawalipi kodi na pia hawaji kwa wingi nchini Baba umeanzisha kodi, umeisimamia ilipwe na inalipwa na bado watalii wameongezeka kwa asilimia 10;

3. Ndani ya mwaka mmoja umeenda kasi na wapiga dili; mambo ya hewa hewa katika kila kitu-wafanyakazi hewa, waajiri hewa, walimu hewa, wanafunzi hewa, zabuni hewa, malipo hewa, wanasiasa hewa na hata walalamishi hewa wote wanajua kinachowatokea.

Yani hapa Baba umefanya ka Darasa "Weka muziki sitaki maneno."😂😂😂

4. Baba unatuchanganya hii miradi mikubwa unayoenda nayo kasi hivi tena ndani tu ya mwaka mmoja hatukuelewi ujue-reli ya kisasa umeshatangaza zabuni, Tazara na Ocean Road unajenga barabara za juu tayari, mgonjwa wetu ATC si tu kaamka bali naye kaanza kunata na bit ya Darasa, ushaleta ndege 2 na unaleta 4 zaidi ikiwemo Boeing Dream-liner Mzee please... Mzee taratibu;

5. Baba baba khaaa! mfumuko wa bei umerudi digit moja, kodi ya mishahara umerudisha digit moja jamani hatujazoea haya ujue Baba;

6. Kale kawimbo ketu ka miaka mingi ka ugonjwa wa kutochukua hatua umekazima-wakifanya fyuu tu umetumbua sasa tunalalamika na kawimbo ka "hufuati sheria" ingawa nako kamepigwa redioni mara mbili tu kamezimwa. Nakatafuta sijakasikia tena;

7. Kuna kaugonjwa kengine Baba umekatibu duh! daktari kweli wa kemia. Watu walizoea siasa siasa tu kila mahali, bla bla na kutokufanyakazi bali kuandamana tuu mabarabarani sasa ni kazi tu na hadi yule mzee wa watu kakiri eti "anafurahia mikutano ya ndani,"Baba wewe mbaya!!!

8. Kuna watu Baba walikuwa wanajua Tanzania ni shamba la bibi wanakuja na kampuni za mifukoni na kuondoka na mabilioni kwenye sandarusi leo wanalalamika balaa ujue.

Wanakuja wale tu wenye nia thabiti ndani ya mwaka mmoja tu yani wamekuelewa. Khaa! Baba hii karama umepata wapi Baba;

9. Nikipita mikoani naona maumeme tu watu wanaunganishiwa naona mabomba tu ya maji miradi inakamilika. Baba unaenda kasi mno Baba khaa!!

Miaka 10 kwa kasi hii Baba si tutakuwa Manhattan sasa. Unajua hatujajiandaa Baba oooh!!

10. Unajua Baba ngoja nikwambie kitu... najua unapumzika kijijini ukitafakari.

Nilitaka kukwambia neno hili tu na ulikumbuke 2017 tena naomba nikunong'oneze: "Unatuangusha Baba, kasi hii wenzio hatujazoea ujue. Tunajitahidi kuzoea please usituangushe, ukiiacha tu umetuua hatutaweza tena kurejea kwenye yale mazoea yetu.

Wako Hadija wa Singeli, Kitaani Mbagala Kuu jijini Dar.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu