Natumia ukurasa huu kumpongeza Jenerali Ousman Badgie ambaye ndiye mkuu wa majeshi nchini Gambia (Head Of Gambian Army) kukataa vikosi vyake kupigana na vikosi vya Umoja wa nchi za Afrika Magharibi kwa kifupi (ECOWAS).

Jenerali Ousman ameiambia AFP kuwa kamwe hawezi kuamuru vikosi vya Jeshi nchini mwake Gambia vipigane na vikosi vya ECOWAS kwa interest za kisiasa sitaki kuona raia wa Gambia akiumizwa au kuuwawa kwa sababu za kisiasa'' alisema Jenerali Ousman.

Kwa tafsiri ya haraka ni kwamba Jenerali Ousman ameheshimu matakwa ya wananchi wa gambia waliomchagua bwana Barrow kutoka chama kikuu cha upinzani kuwa rais wa nchi hiyo. Kwa maana fupi ni kwamba Jenerali ousman hayupo tayari kumlinda dikteta Yahya Jammeh rais aliyeshindwa uchaguzi na kumaliza muda wake kisha kung'ang'ania madaraka.

Kwa Afrika hii huyu ndiye mkuu wa majeshi wa kwanza kuwa upande wa wananchi nampongeza sana na anapaswa kutunzwa tuzo ya nobel na sina uhakika kama Afrika yote kuna mkuu wa majeshi mwenye moyo na maamuzi chanya kwa taifa kama huyu.

Tumekuwa na wakuu wa majeshi wengi africa ambao mara zote huungana na madikteta kuumiza, kutesa na kuuwa wananchi.

Kwa kauli hii ya mkuu wa majeshi gambia utavirahisishia vikosi vya ECOWAS kumuondoa haraka dikteta yahya jammeh anayeng'ang'ania madaraka huku tayari kuanzia juzi ameondoa mke na watoto kuwapeleka nchi za ng'ambo na kubaki yeye ili awaumize na kuwauwa wake na watoto wa wagambia wenzake..

Lakini pia nizipongeze nchi wanachama wa ECOWAS ambazo ni muunganiko mwa nchi za Afrika Magharibi kwa kusimamia demokrasia siku zote demokrasia ikikua na uchumi unakua. Hatua mliyochukua kwenye jumuiya yenu ya kumuondoas rais anayeng'ang'ania madara sizani kama EAST AFRICA au SADEC kama wanaweza kuchukua hatua kama hiyo zaidi ya kumsaidia yule anayeng'ang'ania madaraka.

Mdude Nyagali
Sumu ya Nyigu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: