Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Iringa Josephina Mwaipopo akiwa na mtoto aliyebakwa.
DC Richard kasesela akiwa amemnyanyua mtoto aliyebakwa akitoka nae kuchukuliwa vipimo Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
Watuhumiwa baba na mwanae wakiwa chini ya ulinzi.

Na MatukiodaimaBlog

Jeshi la Polisi likiongozwa na mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wamefanikiwa kumkamata kijana Emmanuel Mkiwa (19) kwa tuhuma za kumbaka mara kwa mara mdogo wake wa miaka (4).

Imedaiwa kuwa kijana huyo ambae ni mwenyeji wa mtaa wa Omary Matrekta kata ya Mtwivila katika Manispaa ya Iringa alikuwa akiishi nyumba moja na babake pamoja na wadogo zake watatu wawili wa kiume na mmoja ni mtoto huyo wa miaka 4 ambaye alitelekezwa na mamake mzazi kutokana na mambo ya kifamilia kati yake baba wa mtoto.

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea January 16 majira ya saa 2 usiku walimweleza mwandishi wa Matukio Daima blog kuwa kijana huyo mara kwa mara alikuwa akimbaka mdogo wake ambae baba mmoja na mama tofauti kabla ya mtoto huyo kuwaeleza majirani kuwa kakake huyo amekuwa akimkandamiza na kijiti sehemu zake za siri (akimbaka).

Kutokana na maelezo ya mtoto huyo ndipo taarifa za raia wema hao zilipofikishwa kwa mkuu wa wilaya na kuamua kufika katika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata kijana huyo na baba mzazi wa watoto hao Shukuru Mkiwa kwa malezi mabaya ya watoto.

Akizungumza baada ya kukamatwa kwa kijana huyo mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na kuwashukuru raia wema kwa kufikisha taarifa ya kunyanyaswa kwa mtoto ila aliendelea kutoa wito kwa wananchi wengine ambao wanataarifa za kunyanyaswa kwa mtoto yeyote katika wilaya ya Iringa kutoa taarifa ili wahusika wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Kasesela alisema kuwa uchunguzi uliofanywa baada ya vipimo katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa umeonyesha mtoto huyo kashaondolewa usichana wake na hivyo kulazimika kulazwa kwa matibabu katika Hospitali hiyo huku akiahidi kumsaidia mtoto huyo kumsomesha.

Japo alisema alishangazwa na hatua ya baba mzazi wa kijana huyo kumficha mbakaji ndani na kudanganya kuwa hayupo wakati kijana wake alikuwepo ndani hivyo mzazi huyo kukamatwa pamoja na kijana wake yeye kwa kosa la kumchifa mharifu na kijana wake kwa kosa la ubakaji.

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa kupitia kwa kamanda wa polisi mkoa (RPC) Julius Mjengi limethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kuwa baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani huku likiwataka wananchi kuendelea kufichua waharifu zaidi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: